• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YANUNUA PIKIPIKI 7 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 23 KWA AJILI YA KATA ZA PEMBEZONI.

Posted on: March 31st, 2020

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imenunua Pikipiki saba (7) aina ya YAMAHA zenye thamani ya Shilingi Milioni 23,100,000/= pamoja na kodi (VAT) kupitia fedha za Mradi wa uboreshaji Miji (ULGSP) katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya kuwajengea uwezo Watumishi kwa kuboresha utendaji kazi wao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  mara baada ya makabidhiano hayo ya Pikipiki ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema Pikipiki hizo zimenunuliwa  mahsusi kwa ajili ya Kata za Pembezoni ambazo Pikipiki nne  (4) wamepatiwa Kata za Luhungo, Mzinga , Mkundi pamoja na Kingolwira.

Amesema Pikipiki tatu (3) zimebakia Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Halmashauri.

“Tunaipongeza sana Manispaa kwa kuwa na jicho la tatu kununua Pikipiki hizi, Kata hizi za pembezoni zinachangamoto sana haswa kwa Watendaji wake wanashindwa kuwafikia Wananchi kwa urahisi na kushindwa kutoa huduma  lakini kwa hiki walichokifanya kitatoa mwanya mzuri wa Watendaji kuwahudumia wananchi wao ipasavyo, lakini niwaombe na kumuomba Mkurugenzi wetu wa Mansipaa kwamba Pikipiki hizi zitumike katika muda wa kazi baada ya hapo wewe  mtendaji endelea na mambo yako mengine weka chombo hicho nyumbani kwani isijekuwa Manispaa imefikiria kuleta maendeleo harafu maendeleeo hayo yakageuka vifo tunajuana tabia zetu sasa tuvilinde na kuvithamini”Amesema Mhe. Kihanga.

Hata hivyo amewataka Watendaji wa Kata hizo, kuvitumia vyombo hivyo vya Moto kwa malengo yaliyokusudiwa na sio kuvitumia kwa ajili ya kugeuza kuwa Bodaboda na kujipatia kipato kwa atakaye kiuka utaratibu atachukuliwa hatua za Kisheria .

Katika hatua nyingine, amewapongeza Wataalamu wa Manispaa na kuwaomba mara baada ya Miradi iliyopo kukamilika waanze kufikiria miradi mipya kwani anaamini Bajeti ijayo ya Mwaka wa fedha wa 2021/2022 Manispaa itakuwa na fedha za kutosha na kuweza kuwa na bajeti kubwa ya kihistoria.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema Manispaa imetoa Pikipiki hizo kwa ajili ya kurahisisha huduma kwa Wananchi na kuhakikisha huduma bora zinapatikana katika Kata hizo.

Amesema kuwa  matarajio yake ni kuona kuwa Pikipiki hizo zinarahisisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Serikali kwani hata maeneo yasiyofikika kwa urahisi kwa gari sasa yatafikika.

“Tuvitunze vyombo hivi, Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, imeonyesha moyo wa kuthamini kazi zetu nasi tuvipe heshima na kuvitumia kwa malengo tarajiwa, tusiende kuvigeuza Bodaboda na tutaweka utaratibu yule ambaye atakiuka utaratibu huu tutamchukulia hatua kali za kisheria niwaombe Watendaji chapeni kazi tuendelee kuwahudumia Wananchi wetu katika Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika kufikia adhima ya Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati”Amesema Sheilla.

Aidha, Mkurugenzi amewataka Watumishi wote wa Manispaa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo na kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DKT.KIJAJI AFUNGA WIKI YA MAZIWA KITAIFA NA KUWATAKA WAFUGAJI KUZALISHA MAZIWA SALAMA KUENDANA NA USHINDANI WA SOKO LA MAZIWA.

    June 02, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUSAFISHA MAZINGIRA YAO MARA KWA MARA

    May 31, 2025
  • WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE

    May 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa