• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu, na Usimamizi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MEYA KIHANGA AWACHARUKIA WAALIMU WAKUU, AWATAKA WAJITATHIMINI

Posted on: January 19th, 2021

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Walimu wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, kujitathimini na kuona Kama wanafaa kukaa Manispaa Morogoro.

Kauli hiyo ameitoa Januari 19, 2021 wakati wa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa vilivyojengwa na Manispaa Morogoro na nguvu za wananchi  kufuatia agizo la Serikali la kutaka wanafunzi wote kuingia darasani ifikapo Februari 28.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Kihanga, amesema kumekuwa na matokeo mabovu ambayo hayaridhishi jambo linalopelekea Manispaa kushika nafasi za nyuma huku ikiwa mjini.

Mhe. Kihanga, amesema kuwa, sasa ni wakati wa Waalimu hao kuanza kujitathimini upya kutokana na matokeo hayo.

" Nimeanza ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Shule na vyumba vya Madarasa, lakini matokeo bado hayaridhishi hususani katika upande wa Sekondari, tunashindwa hadi na wenzetu wa vijijini, sisi tuna kila kitu ila ni wapi tuna kwama? Hizi nafasi sio zetu, niwaombe Waalimu mjitathimini, Serikali inawekeza katika ujenzi na sisi tunataka matokeo mazuri, baada ya ujenzi wa madarasa tunahamia kwenu, kama umeshindwa kukaa Manispaa ondoka kabisa, tunataka matokeo mazuri tufanane na hadhi yetu ya Manispaa" Alisema Mhe.Kihanga.

Aidha aliwataka Waalimu wakuu wanapokaa katika vikao vyao wamualike ili wazungumze kwa pamoja na kuona changamoto ambazo zipo na kuzitatua. Suala la Waalimu amesema kuwa mpango uliopo kwa sasa ni kuongeza Waalimu wa Sayansi ambao ndio changamoto kwa Sasa. Kuhusu Ujenzi wa Shule ya Msingi Konga, amempongeza Sana Mkurugenzi Manispaa Morogoro Sheilla Lukuba, kwa jitihada za kupambania Sekta ya elimu, kwani Sasa amekuwa akitoa fedha nyingi katika kata kwa ajili ya maendeleo mbalimbali ikiwemo sekta ya  elimu.

" Mkurugenzi wetu anajitahidi Sana , tumtumie vizuri, anahangaika Sana, sisi hatuhitaji kubweteka, tufanye kazi, haya matokeo yanatuumiza Sana, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wote tunaumia, huu ni muda wa kujipanga sasa tutoke hapa tulipo twende mbele"Aliongeza Mhe. Kihanga.

Mwisho , amesema kuwa ziara hizo zitakuwa endelevu, lakini kwanza ameanza katika Shule za Sekondari baada ya hapo atahamia Shule za Msingi. Miongoni mwa Shule alizoanza nazo ziara ni pamoja na Shule ya Msingi Konga Kata ya Mzinga, Shule ya Sekondari Kihonda Kata ya Mazimbu, Shule ya Sekondari Sumaye Kata ya Bigwa na Shule ya Sekondari Lupanga Kata ya Kilakala.

Naye Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, amemshukuru, Mstahiki Meya kwa ziara hiyo huku akimuahidi kumpa ushirikiano na kuhakikisha anafuatilia kwa ukaribu maswala ya elimu katika Kata hiyo.

Matangazo

  • HERI YA SIKUKUU ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA WA 2021 December 24, 2020
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA WATENDAJI WA MITAA DARAJA LA TATU TAREHE 20/6/2020 June 12, 2020
  • TANGAZO LA UCHAGUZI MKUU October 20, 2020
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA WANAOTAKA KUPANGA VIOSKI MANISPAA YA MOROGORO March 25, 2020
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • MANISPAA MOROGORO YAIBUKA KINARA WA LISHE MKOA WA MOROGORO

    February 05, 2021
  • WANANCHI WATAKIWA KUENDELEA KUSHIRIKI KATIKA UJENZI WA MADARASA

    January 28, 2021
  • WAITARA ARIDHISHWA NA USAFI MANISPAA YA MOROGORO, ATAKA KASI IONGEZWE KATIKA UPATIKANAJI WA DAMPO LA KISASA

    January 25, 2021
  • MEYA KIHANGA AWACHARUKIA WAALIMU WAKUU, AWATAKA WAJITATHIMINI

    January 19, 2021
  • Angalia Yote

Video

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MANISPAA YA MOROGORO WAZIRI KOMBO ATANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ULIOFANYIKA NOV.24/2019.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa