• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DAS WILAYA YA MOROGORO ATOA WITO KWA TAASISI MBALIMBALI KUJITOLEA KUSAIDIA WATU WENYE UHITAJI MAALUMU

Posted on: June 17th, 2020

KATIBU Tawala Wilaya ya Morogoro, Ruth John, ametoa wito kwa taasisi mbalimbali, mashirika, wafanyabiashara na watu wenye mapenzi mema kujitolea kusaidia watu wenye uhitaji maalumu kwani kwa kufanya hivyo ni kutimiza amri kuu ya upendo ya Mwenyezi Mungu isemayo pendaneni kama mimi nilivyowapenda ninyi.


Ruth ameyasema hayo akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo wakati akitoa misaada mbalimbali kwa Makao ya kulelea watoto wenye mahitaji maalumu Mgolole pamoja na Mission To The Homeless katika hafla fupi ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Juni 16,2020.

 


 

DAS Ruth , amekabidhi misaada hiyo kwa wawakilishi wachache wa watoto hao walioongozana na baadhi ya walezi wao, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo la serikali la kuepuka mikusanyiko ya watu isiyo lazima kutokana na janga la ugonjwa wa mafua makali ya CORONA.

 


 



 "Mkuu wa Wilaya yenu anawapenda sana , ameniagiza nije kuwaona na kuwaletea kile alaichokiandaa , kwahiyo niseme kuwa Serikali yenu chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli inawapenda sana , kikubwa mjisikie huru kama walivyo watoto wengine, msirudi nyuma kwani kuondokewa na Wazazi au kukosa malezi ya wazazi isiwe kigezo cha kuwarudisheni nyuma mnatakiwa msongo mbele ili nanyi myafikie malengo mliyojiwekea" Amesema Ruth.

Aidha amesema kuwa wapo watu ambao wamekuwa wakitoa misaada kwa watoto au watu ambao wamekua wakizunguka mitaani na kuomba misaada kuwa, huo sio utaratibu mzuri na kusisitiza kuwa ni vyema mtu unapokuwa na tatizo na unahitaji msaada kufika katika ofisi za serikali na kuonana na Maafisa Ustawi ili waweze kushauri njia bora za kuweza kusaidiwa.

Kwa upande wa Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Enedy Mwanakatwe, amesema ni vyema jamii ikawiwa kuchangia makundi ya watoto wenye mahitaji maalumu vikiwemo vituo vya watoto yatima kwani kundi hili linahitaji msaada wa kuwa karibu zaidi na jamii kutokana na wengi wao kupotelewa na wazazi au kutelekezwa na ndugu zao.

Mwanakatwe, amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya ndugu wa watoto waliopo kwenye vituo na jamii kwa ujumla kutokuona umuhimu wa kuwatembelea na kuwajulia hali watoto licha ya elimu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara kwa kuona kuwa jukumu hilo ni la jamii kwa ujumla na sio Serikali peke yake au taasisi binafsi.

“Pindi inapotokea mtoto amefiwa na wazazi ndugu wamekuwa wakiwaleta watoto vituoni, watoto wakishapokelewa ndio mwisho wa ndugu wa mtoto husika kufika kituoni kumjulia hali au pengine hata kusaidia mahitaji mbalimbali, jambo hili linasikitisha sana mtoto anakua pasipo hata kufahamu ndugu zake wakati hii ni haki ya mtoto kisheria.”Amesema Mwanakatwe.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, ametoa rai kwa wamiliki wa vituo vya kulelea watoto kuhakikisha kuwa pindi wapatapo taarifa au wanapoletewa watoto waliotelekezwa au kupotelewa na wazazi ni vyema kufikisha taarifa kwa maafisa ustawi kabla ya kuwapokea na kuanza kuwahudumia katika vituo vyao lengo ikiwa ni kuhakikisha kuwa Maafisa ustawi wanashirikishwa ili waweze kufuatilia kwa undani taarifa za watoto husika lakini pia kujua taarifa za awali za mtoto husika kwani kumekuwa na tabia ya wazazi kutelekeza watoto wakiamini kuwa watasaidiwa vyema kwenye vituo vya kulelea watoto jambo ambalo sio sahihi.


Sidina amesema kuwa kwa mujibu wa sheria namba 21 ya mwaka 2009 kifungu namba 94 kinaeleza wajibu wa Halmashauri kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

 Misaada aliyotoa Katibu Tawala ni pamoja na mchele kilo 200, mafuta ya kula lita 80 na Sukari Kilo 50 kwa makao yote mawili.

 


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa