• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu, na Usimamizi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Public Relation
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO YAIDHINISHA SHILINGI BILIONI 95.6 MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Posted on: February 25th, 2023

BARAZA la Madiwani Manispaa ya Morogoro imeidhinisha kutumia kiasi cha shilingi 95.690,984,212.00 katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani la kupitisha mpango na Bajeti ya Manispaa ya Mwaka 2023/2024.

Akizungumza katika Baraza hilo, Mhe. Kihanga, amesema , matumizi hayo yamepanda kwa asilimia 13.16 ya matumizi ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo mwaka wa 2022/2023 Manispaa ilitumia kiasi cha shilingi 87,256,281,250.00.

Mhe. Kihanga ,amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa fedha za mishahara ya ajira mpya na promosheni ya watumishi ambapo mishahara ni Bilioni 72,071,194,000.00, matumizi mengineyo Bilioni 1, 152,173,000.00, miradi ya maendeleo shilingi Bilioni 9,639,944,669.00, na Shilingi Bilioni 12,813,917,512.00 ya mapato ya ndani.

Miongoni mwa vipaumbele vya bajeti ya mwaka 2023/2024 ambavyo Mhe. Kihanga amevitaja ni pamoja na Kumalizia tatizo la madawati sekta ya elimu Msingi na Sekondari, kuhamisha machinjio ya Manispaa kwenda Kata ya Mkundi, kumalizia miradi viporo ndani ya Manispaa ikiwamo Ofisi za Kata na Mitaa, Kuanzisha ujenzi wa Ofisi Mpya ya Manispaa kuijenga Kihonda (SGR), Kuanzisha ujenzi wa Ukumbi mkubwa na Hotel katika eneo la Gymkhana, kumalizia maboma 50 ya madarasa ya kiushindani shule za msingi , kufungua barabara mpya na kukabidhi TARURA ndani ya Manispaa kwa kununua Greda, kuanzisha mradi wa kununua , kufidia na kuuza viwanja , Ujenzi wa Vyumba 2 vya upasuaji Vituo vya Afya Mafiga na Sabasaba, kumalizia miundombinu ya Zahanati ya SINA, Kufanya ukarabati Zahanati ya Mji Mpya, kumalizia ujenzi Kituo cha afya Tungi, Kumalizia na kuongeza miundombinu ya shule ya Sekondari ya Ghorofa Boma, kumalizia majengo ya elimu ya sekondari ya Lukobe na Mindu, Utoaji wa mikopo asilimia 10 kwa makundi maalum Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu pamoja na kuboresha miundmbinu ya machinga na vitega uchumi vya manispaa kwa lengo la kuongeza mapato.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Mhe. Rebeca Nsemwa, amesema mapendekezo ya Bajeti yamelenga kutatua changamoto za wananchi pamoja na kufanikisha ndoto ya Manispaa kuwa Jiji.

DC Nsemwa, amewataka Madiwani pamoja na watumishi wa Manispaa ya Morogoro kuwa kitu kimoja ili kuweza kufanikisha kwa ufanisi bajeti ambayo inakwenda kupitishwa ya mwaka 2023/2024.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amewaambia Madiwani waendelee kuwaamini wataalamu huku akiwaahidi kuitekeleza Bajeti hiyo na kuifanya ndoto ya Manispaa kuwa Jiji inakamilika.



Matangazo

  • TANGAZO LA UUZWAJI VIWANJA ENEO LA KIEGEA A NA B December 02, 2022
  • ORODHA YA MADEREVA NA WATENDAJI WA MITAA DARAJA LA III WALIOITWA KUFANYA USAILI TAREHE 29/08-1/09/2022 August 22, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 06, 2022
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • DC NSEMWA AWATAKA WADAU WA SANAA KUCHANGAMKIA MKOPO WA ASIMILI 10 WA HALMSHAURI

    March 10, 2023
  • KATA YA SABASABA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE UHITAJI.

    March 07, 2023
  • MBUNGE MZERU AAHIDI MILIONI 1.5 KUTUNISHA MFUKO WA JUKWAA LA WANAWAKE KIHONDA KUJIKWAMUA KIUCHUMI.

    March 07, 2023
  • DIWANI CHOMOKA KUJA NA MKAKATI WA KUVISAIDIA VIKUNDI KUPATA MASOKO.

    March 06, 2023
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa