• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

BMK MAFIGA YAKABIDHI MIRADI YA MADARASA NA MAKTABA VYENYE THAMANI YA MILIONI 150 KWA KAMATI YA SIASA YA KATA

Posted on: April 28th, 2023

BARAZA la Maendeleo Kata ya Mafiga chini ya Mwenyekiti wake ambaye ndiye Diwani wa Kata hiyo, Mhe. Thomas Butabile, wamekabidhi miradi ya shule ikiwemo Maktaba ya Shule ya Sekondari Mafiga pamoja vyumba vipya vya madarasa Shule ya Msingi Mafiga B.

Akizungumza katika mapokezi hayo ya miradi hiyo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Mafiga, Ndg. Juma Habibu, amesema, wao kama wasimamizi wa Ilani ya Chama, wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kubariki kuendelea kutumika kwa ajili ya kutoa huduma.

Aidha, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ,Ally Machela, kwa kushirikiana na timu ya Wataalamu kwa kuitekeleza vizuri ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo.

Hata hivyo, amempongeza Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe. Thomas Butabile na timu yake ya BMK kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na kuweza kuifanya Mafiga iwe na ongezeko la kimaendeleo.

Naye Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, amesema katika ujenzi wa madarasa hayo mapya shule ya Msingi Mafiga B, Ofisi ya Kata ilipokea shilingi Milioni 67,376,180.00 na kupokea tena milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maktaba Shule ya Sekondari Mafiga.

Aidha, Mhe. Butabile, amesema hadi kukamilika kwa majengo hayo kutasiaidia kuimarisha huduma za elimu na ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi.

Amesema kuwa katika madarasa ya Shule ya Msingi Mafiga B, zaidi ya milioni 67,376,180 zimetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi zimetumika katika ujenzi huo ambapo ujenzi wa jumla umegahrimu milioni 109,170,410.00 ambapo shilingi milioni 40,775,880.00 ni fedha za nguvu ya wananchi na wadau wa maendeleo, milioni 2,244,200.00 michango ya wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo.

Butabile ,amesema kukamilika kwa mradi wa madarasa kutasaidia kupunguza changamoto ya msongamano wa wanafunzi darasani, kuongeza ari ya wanafunzi na waalimu katika ufanisi wa kujifunza, pamoja na kuongeza ufaulu shuleni kutokana na mazingira rafiki ya kujifunzia.

Hata hivyo,amesema safari haijaishia hapo kwani mpango uliopo ni kuhakikisha wanakwenda kukamilisha ujenzi wa madarasa 3 na Ofisi katika Shule ya Msingi Misufini B , Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata, nyumba ya mwalimu wa shule ya Msingi Mafiga B , Maabara ya Kituo cha afya cha Mafiga ambapo miradi yote hiyo inasubiri fedha za umaliziaji kutoka Halmashauri.

Upande wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Mafiga, Amina Saidi, amewapongeza wazazi pamoja na wadau wa maendeleo kwa kufanikisha ujenzi wa madarasa hayo mapya huku shukrani za kipekee akizielekeza kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kutoa fedha hizo za ujenzi wa madarasa.

"Ujenzi huu hatujaufanikisha peke yetu, tunakishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kusimamia vyema Ilani ya Chama , namshukuru Diwani wetu kwa kuwa bega kwa bega usiku na mchana, nawashukuru sana watendaji wenzangu, wazazi, wadau wa maendeleo wakiwemo wafanyabiashara wa ndani na nje ya Kata yetu, Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa kujitoa kwa hali na mali katika kufanikisha ujenzi unafikia hatua ya kupata fedha za umaliziaji" Amesema Amina.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa