• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC CHONJO AAGIZA MKATABA WA UJENZI WA STENDI YA DALADALA KUANGALIWA UPYA.

Posted on: October 30th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo ameuagiza uongozi wa Manispaa kupitia upya gharama za ujenzi  wa stendi ya daladala ambazo ni  shilingi bilioni 5.2 ili kujiridhisha kama fedha hiyo inaendana na ukubwa wa mradi.

Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo Oktoba 29 mara baada ya kufanya ziara ya kukagua mradi huo  na kutoa  agizo hilo ambapo pamoja na kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi ametilia shaka gharama ya ujenzi  zilizobainishwa kutokana na aina ya majengo yanayojengwa katika eneo hilo la stendi.

Akitoa taarifa mbele ya DC,Mtaalamu  mshauri wa mradi Antonio Mpinga kutoka kampuni ya Howard Humphrey ameeleza ujenzi wa stendi hiyo utagharimu kiasi cha Bilioni 5.2 ambapo jengo la utawala litagharimu zaidi ya mil 400,Jengo la vyoo Tsh Mil 256,stoo Tsh Mil 40.

DC Chonjo ameeleza kusikitishwa na ukubwa wa gharama hizo na kueleza kuwa tukumbuke kuwa fedha hizo ni za mkopo na zitatakiwa kurejeshwa hivyo tuwe wazalendo kwa nchi yetu na wakandarasi wawe wanaandika bei zinazoendana na ukweli na amewaagiza TAKUKURU kukagua mikataba iliyopo na kujiridhisha na matumizi ya fedha.

Aidha Chonjo amemwagiza mkurugenzi wa Manispaa kuangalia upya mikataba hiyo na kuhakikisha inaendana na hali halisi,pia amemwagiza mkandarasi anajenga kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla ya tarehe 31 Desemba.

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi,Dc Chonjo pia amekagua miradi mingine miwili ya elimu katika shule ya msingi Azimio na sekondari ya Kingolwira ambazo zimepata fedha za fidia kutoka SGR baada ya maeneo ya shule hizo kuchukuliwa kwaajili ya ujenzi wa reli ya kisasa na kueleza kuridhishwa na kazi zilizofanyika kwa kutumia fedha hizo.

Baada ya ukaguzi Chonjo ameuagiza uongozi wa shule  ya sekondari kingolwira kuhakikisha wanaanza ujenzi wa uwanja wa michezo kwaajili ya wanafunzi na kusisitiza kuwa serikali inatoa fedha ili kuona matokeo mazuri ya kazi.




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa