• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC CHONJO ATOA MASAA 24 KWA WATENDAJI AMBAO HAWAJAWASIRISHA FEDHA ZA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI KUFIKISHWA MAHAKAMANI

Posted on: December 16th, 2019

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, ametoa masaa 24 kwa Watendaji wote ambao hawajawasirisha pesa za Vitambulisho vya Wajasiriamali vilivyotolewa na Mhe.Rais  Dkt.John Magufuli  kufikishwa mahakamani pamoja na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Desemba 16, 2019, Ofisini kwake, amesema awali watendaji  wa kata walikuwa wanadaiwa Jumla  ya Shilingi Milioni 10,440,000/=  lakini baada ya kuanza ufuatiliaji  na kuwaweka  ndani walirudisha na kubakiza  Shilingi Milioni 5,510,000/=.ambazo hazijawasilishwa hadi leo.

DC Chonjo amesema kuwa, Manispaa ya Morogoro ilipokea jumla ya Vitambulisho  14,146 kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ambapo kwa kata zote 29 kila Mtendaji aligawiwa, hivyo katika marejesho ni watendaji 3 (watatu) ndio hawakurejesha pesa hizo aidha kwa njia ya TRA wala ngazi ya   Manispaa.

Amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 Desemba 2019, jumla ya Vitambulisho 12636 vyenye thamani ya Shilingi milioni 257,741,000/= viliuzwa kwa Wajasiriamali ambapo Vitambulisho 275.5 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 5,510,000/= fedha zake bado hazijawasilishwa .

Miongoni mwa  Watendaji ambao hawajarejesha pesa hizo ni pamoja na Godfrey Maumba  mtendaji wa kata ya Kichangani ambae anadaiwa Vitambulisho 154 anayedaiwa Shilingi Milioni 3,080,000/=, Maxmilian Makota Mtendaji Kata ya Mbuyuni alichukua Vitambulisho 113.5 anadaiwa Milioni 2,270,000/= na Cecilia Kolukwi Vitambulisho 8 anadaiwa Shilingi 160,000/=.

"Vitambulisho vyote tulivyowagawia  vilionekana vimeuzwa na pesa wametafuna,  Tumejitahidi kuwaita wahusika lakini bado pesa hizo mpaka sasa hawajazirejesha, Afisa utumishi nakuomba hawa watu baada ya kurudisha hizi pesa wachukuliwe hatua kali za kinidhamu, Mhe. Rais ametoa vitambulisho hivi kwa nia njema pamoja na kuwapa heshima Wajasiriamali na kuongeza pato la Taifa sio fedha kuliwa kiholela , nataka mpaka kesho saa 4:00 Asubuhi pesa hizo ziwe zimewasilishwa TRA la sivyo wafikishwe mahakamani haraka sana" Amesema DC Chonjo.

Mbali na Manispaa ya Morogoro, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmsahuri ya Morogoro Vijijini kuhakikisha pesa zote za vitambulisho zimepelekwa TRA na wale ambao bado hawajarejesha pesa hizo kwa kuzitumia kwa matumizi yao binafsi watafikishwa Mahakamani na kuchukuliwa hatua  za kinidhamu baada ya kurejesha pesa hizo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema amepokea agizo la Mkuu wa Wilaya hivyo wanakwenda kulifanyia kazi ili kuhakikisha wale waliokula pesa za Vitambulisho wanafikishwa Mahakamani haraka iwezekavyo.

Amesema Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuleta mabadiliko hivyo amewataka Watendaji waachane na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea badala yake wajikite katika kutoa huduma bora ikiwamo kuzingatia miiko ya kazi na uadilifu kazini.

"Watendaji wasio wazalendo na nidhamu katika nchi hii kiukweli hawatufai tunataka watendaji wenye moyo wa kizalendo, waadilifu na waaminifu kwa ajili ya kulitumikia Taifa kwa ajili ya kuwaletea Wananchi maendeleo nasiyo wao wajilimbikizie mali na kunufaisha matumbo yao, tunahitaji matokeo chanya, Rais wetu Mhe. Dkt John Magufuli ameonesha dhamira ya dhati ya kuwakwamua Wajasiriamali hivyo lazima nasisi tuwe na huruma ya kumsadia kutimiza adhima yake katika kuelekea uchumi wa kati wa Tanzania ya Viwanda" Amesema Sheilla

Ametoa wito kwa Watumishi wote, ikiwamo Wakuu wa Idara, Watendaji wa Kata pamoja  na wa Mitaa waweke uzalendo mbele hususani katika masuala mazima ya maendeleo na mipango mikubwa ambayo Mhe. Rais anaidhamiria kwa Wananchi wake.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa