• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC CHONJO AZINDUA MAPIPA 50 YA TAKA YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 591 MANISPAA YA MOROGORO

Posted on: January 28th, 2020

MKUU a Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, amezindua mapipa  ya kuhifadhia takataka(skipbacket) 50  yenye thamani ya Tsh 591,519,500  ambapo kwa leo  jumla ya mapipa 35 yenye thamani ya Tsh 414,063,650.00 ameya pokea   ikiwa ni awamu ya kwanza ambapo Manispaa ya Morogoro ilitenga jumla ya Tsh 591,519,500 kwaajili ya ununuzi wa mapipa 50.

Zoezi hilo limefanyika leo Januari 18, 2020, katika Viwanja vya Kata ya Mji Mkuu, ambapo amewataka wanachi kuvitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Amesema Manispaa ya Morogoro, ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya kutokuwa na Mapipa ya kuhifadhia taka ya kutosha, ambapo awali yalikuwa 30 na mahitaji ni mapipa 100.

Amesema Mapipa hayo yametumia jumla ya Shilingi Milioni 591 kila pipa likiwa na thamani ya shilingi milioni 11 na kusababisha mapipa kuwa na mapipa 65 huku mapipa 35 yakiwa yamezinduluiwa leo.

Amesema kwa awamu ya kwanza , mzabuni wa PUMA LOGISTICS SOLUTION LTD, aliyekuwa amepewa kazi hiyo amekabidhi mapipa 55 yenye gharama ya shilingi Milioni 414 ambapo mapipa 15 yaliyobakia yatakabidhiwa mara baada ya kukamilisha kuyatengeneza.

Äidha, amesema Mapipa hayo yatagawanywa katika Masoko, maeneo yenye msongamano wa watu, maeneo yenye shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii.

Mara baada ya Mapipa hayo kujaa taka yatakuwa yanabebwa na gari tatu za Manispaa aina ya 'Skip Loader' ambapo Manispaa imeagiza magari mengine 2 ya aina hiyo kwa ajili ya uondoaji wa mapipa ya taka.

"Mapipa haya yataboresha usafi wa mji kwani wananchi watakuwa na sehemu ya kuwekea /kuhifadhi taka zao kwa muda badala ya kuzitupa hovyo au kuziweka kando kando ya barabara, niwaombe wananchi tuendelee kulipa ada ya taka ya kila mwezi ili kuwezesha Kampuni / Vikundi vya usafi na Manispaa Manispaa yetu kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi" Amesema DC Chonjo.

Amesema Morogoro ipo kati kati ya Mji Mkuu wa Makao Makuu ya Serikali Dodoma pamoja na Mji Mkuu wa Biashara Dar Es Salaam, hivyo ili Morogoro iwe Jiji kuna vigezo mmbalimbali ikiwemo suala la Usafi, mandhari husika hivyo kuna haja ya kuwa wasafi.

Pia amewataka Madiwani wa Manispaa ya Morogoro kuhimiza na kusimamia usafi katika kata zao kwa kuwa wao ndio wenyeviti wa Kamati za Maendeleo ya Kata.

 " Mimi nilivyofika hapa Morogoro mwaka 2016 nilikuta kambi ya kipindupindu iliyodumu kwa miaka 5, kuanzia mwezi wa 11 , 2016 kipindupindu kilikuwa ni historia kwa manispaa yetu ya Morogoro, hiyo nayo ni sababu iliyotufanya tuchelewe kuwa Jiji, navitaka  vikundi  vya taka viwajibike kuanzia ngazi za Mitaa na Kata na kama  vitashindwa kufanya vizuri vitafutwe vyene uwezo wa kutatua kero za taka ambapo amesema sio vyema maafisa mazingira kufika katika mitaa yote 294 " Ameongeza DC Chonjo.

Katika hatua nyengine, ameutaka Uongozi wa Soko la Manzese kusimamia uasfi na mazingira kwani soko hilo hariridhishi.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogro, Sheilla Lukuba, amesema fedha za kununulia mapipa ya kuhifadhia taka ngumu wamenunua kupitia fedha za kimkakati ambazo walipatiwa na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli.

Amewataka wananchi kutpotupa taka pembeni badala yake wazihifadhi taka hizo katika vyombo husika na wale watakao kaidi watapigwa faini kwa mujibu wa sheria za mazingira.

Mbali na uzinduzi wa mapipa hayo amesema pia suala la usafi liwe katika damu na sio wananchi wangoje hadi viongozi wafike ndipo wafanye usafi.

" Suala la usafi ni kama unavyooga kila siku, jinsi ya kupiga mswaki bila kusimamiwa, kwahiyo niwasihi wanqanchi wa Manispaa ya Morogoro naomba tufanye usafi bila kushurutishwa , kwani hata Mhe. Rais Dkt John Magufuli amewaonesha Watanzania kwa kliona na kulipa kipaumbele suala la usafi" Amesema Sheilla .

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga,  amesema ujio wa Mapipa ya takataka uendane na usafi wa mazingira.

Mbali na hapo, amesema kuwa sula la usafi katika Soko la Manzese bado ni changamoto na hariridhishi hali iliyomfanya Mkuu wa Wilaya kuwa mkali sana.

Amesema kuwa asilimia kubwa ya wafanyabiashara wanafanya usafi katika sura ya nje lakini katika vizimba vyao kwa chini kumekuwa kuchafu sana jambo ambalo halipendezi na linatakiwa kuchukuliwa hatua ili soko hilo liwe safi.

Amewaomba wafanyabiashara wa Masoko yote yaliyo katika Manispaa ya Morogoro wajitahidi kufanya usafi.

"Tunaweza kuwa na vyombo vizuri vya usafi tukashindwa kufanya kazi zenyewe, amesema kazi hiyo iendelee kufanyika hivyo lakini pia amemuomba Mkurugenzi kufuatilia hayo magari yaliyobakia yaweze kuja mara moja kwa ajili ya kuwasaidia wananchi " Amesema Mhe. Kihanga.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa