• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC KILAKALA AKABIDHI HUNDI YA MILLIONI 699 NA KUGAWA VITAMBULISHO VYA WAMACHINGA.

Posted on: January 11th, 2025

MKUU wa Wilaya ya Morogoro , Mhe. Mussa Kilakala, amekabidhi hundi ya jumla ya kiasi cha Tshs 699,411,000/= ikiwa ni mkopo wa asilimia 10 ya mapato ya ndani,kwa ajili ya makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro sanjari na kugawa vitambulisho vya wajasiriamali wadogowadogo (Machinga).

Zoezi hilo limefanyika Ukumbi wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu.

" Mikopo hii ilisimama kutokana na kuibuka tabia ya vikundi kubadili matumizi ya fedha za mikopo na wengine kukimbia na fedha hizo lakini kuwanufaisha watu ambao sio walengwa wa mikopo,tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha fedha hizi kwenye mfumo mzuri na uliobora ,rai yangu tumieni fedha hizi kwa malengo yaliyokusudiwa sio kwenda kuzichezea ngoma na sherehe, watakaoenda kinyume tutawachukulia hatua kali za kisheria " Amesema DC Kilakala.

DC Kilakala,amesema Dkt.Samia lengo lake ni kuona watu wachini wanajikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao, hivyo amewataka wanavikundi kutorudia makosa yaliyopelekea kusitishwa kwa mikopo hiyo.

Pia,amesema wanawake wamekuwa mfano wa kuigwa katika urejeshaji wa mikopo,amewaomba wakae na Vijana ambao ni watoto wao wawasisitizie juu ya urejeshwaji wa mikopo na watimize malengo ya fedha hizo za mkopo ili wengine waweze kukopeshwa.

Aidha,amewataka viongozi wa Serikali hususani wataalamu wa idara ya mikopo,watumie muda mwingi kuwaelimisha wananchi juu ya vigezo vya kupata mikopo na pale wanapokosea wawasahihishe badala ya kuwarudisha nyumbani.

Hata hivyo, amezitaka kamati za Mikopo kutoa elimu kwa vikundi ambavyo havijakidhi vigezo vya kupata mkopo kwa sasa ili wanakikundi wakamilishe taratibu zote zinazotakiwa kwaajili ya kupata mkopo kwa wakati mwingine.

Katika hatua nyingine,amewahimiza wazazi juu ya malezi ya watoto kutokana na wimbi la ukatili watenge muda wa kukaa na watoto wao badala ya kujikita zaidi kwenye utafutaji wa fedha.

Naye , Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Mikopo ya Wilaya, Hilary Sagara,amesema jumla ya vikundi 55 wamepewa mkopo huo ikiwa vikundi vya Wanawake ni 33, Vikundi vya Vijana ni 15 na Vikundi vya watu wenye Ulemavu ni 07

Kwa upande wa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amezitaka kamati za mikopo kuwa wazi kuielezea jamii taratibu zinazotakiwa kwa vikundi vinavyopaswa kupata mikopo ili kuondoa malalamiko kwa wale watakaokosa mkopo kutokana na kushindwa kuwa na sifa zinazotakiwa.

Akizungumza kwa niaba ya wanavikundi , Nasibu Said, ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, kwa kuwawezesha kupata mkopo utakaotumika kuboresha maisha yao.

Nasibu amesema , watahakikisha wanaendelea kutoa ushirikiano na kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo yao ili kuendeleza zoezi hili kwa wote wenye sifa za kupokea mkopo huo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI YATOLEWA MANISPAA YA MOROGORO.

    May 14, 2025
  • BALOZI BATILDA ATAKA MAONI YA WADAU KUFANYIWA KAZI KUELEKEA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MSHARIKI 2025

    May 06, 2025
  • MAAFISA ARDHI WATAKAOBAINIKA NI VYANZO VYA MIGOGORO YA ARDHI TUTAWAFIKISHA MAHAKAMANI-DKT.NDUMBARO.

    May 05, 2025
  • WAAJIRI SEKTA BINAFSI RUHUSUNI WATUMISHI WENU KUJIUNGA NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI - RC MALIMA.

    May 01, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa