MKUU wa Wilaya ya Morogoro ,Mhe. Mussa Kilakala, ameongoza Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) Manispaa ya Morogoro kikao kilicholenga kujadili mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Manispaa ya Morogoro.
Kikao hicho kilifanyika Januari 31/2025 katika Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo viongozi wa vyama mbalimbali vya Siasa.
Akifungua kikao hicho , DC Kilakala, amesema kuwa kikao hiko kilikuwa na lengo la kujadili mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na kuwaomba wajumbe kupitia vizuri bajeti hiyo kwa maslahi mapana ya Manispaa ya Morogoro na Wilaya kwa ujumla.
Naye , Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Manispaa ya Morogoro,Edward Mwamotela, amesema mwaka wa fedha 2025/2026 Manispaa inakisia kukusanya Shilingi 15,622,877,000.00 ya mapato ya ndani na inakisia kukusanya na kutumia shilingi 93,809,858,854.97.
Mwamotela,amesema mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 yameandaliwa kwa kuzingatia miongozo ,sheria na sera mbalimbali.
Miongoni mwa sera hizo ni Dira ya Taifa ya Maendeleo (2025),Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2021/2022-2025/2026,Sheria ya Bajeti No.11 ya mwaka 20215, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, Mpango Mkakati wa Manispaa ya Morogoro wa mwaka 2021/2022-2025/2026, Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030,Mwongozo na Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2025/2026, Mapendekezo ya Mipango kutoka ngazi ya Mitaa na Kata (O & OD) pamoja na Sera za Kisekta.
Naye Mwenyekiti CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg.Fikiri Juma, amemshukuru DC Kilakala, huku akimuhakikishia kuwa CCM Wilaya ya Morogoro itaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ili wananchi wafaidi matunda ya Serikali yao.
Wajumbe mbalimbali wamempongeza DC Kilakala, na kuwaomba wataalam waendelee kupanga mipango na Bajeti zinazo akisi moja kwa moja uhalisia kwa maendeleo ya Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa