Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mh.Regina Chonjo amefanya ukaguzi wa barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami za Tubuyu na Maelewano zilizopo ndani ya Manispaa ya Morogoro.
Mkuu huyo wa Wilaya akiwa katika ukaguzi huo aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa usimamizi mzuri wa mradi huo ambao hadi sasa umeshatekelezwa kwa asilimia 95.
Aidha Mh.Chonjo amemwagiza mhandisi anayesimamia mradi huo Ndg Godwin Mpinzile kuhakikisha kingo zote za barabara zinawekewa lami nyepesi ili kuepukana na wachuuzi wa kokoto na mmonyoko wa eneo la pembezoni mwa barabara hizo.
Pia ameeleza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na maisha bora hivyo ameagiza wale wote wanaofanya biashara za vyuma chakavu kuacha maramoja kukata mabomba yaliyotumika kuwekea taa za barabarani kwa faida zao binafsi.
"Serikali itamchukulia hatua mwananchi yoyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu"alisema Mh Chonjo
Ameeleza kuwa kila mwananchi anatakiwa kuwa mlinzi wa mwenzake ili kuweza kuitunza miundombinu yetu.
Aidha Mh.Chonjo amemwagiza mkandarasi anayefanya kazi ya ujenzi wa barabara mara amalizapo kazi kufanya usafi ndipo akabidhi kazi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa