MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amewata Wanamichezo na Wasanii waamke kwani huu ni muda muafaka wa kurudisha heshima ya Michezo katika Wilaya ya Morogoro.
Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 02,2020 kwenye kikao cha kukutana na wadau wa Michezo, Sanaa, Elimu na Mazingira Manispaa ya Morogoro kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa kwa ajili ya kujadili changamoto zinazozikumba sekta hizo.
Akizungumza na Waandishi wa habari, DC Msulwa, amesema lazima Morogoro isimame na kurudisha heshima yake katika Nyanja ya michezo, sanaa na utamaduni .
Msulwa, amesema anataka Morogoro ya Viwango katika michezo hivyo ni ngumu kuipata Morogoro ya Viwango kama huwezi kujua changamoto zake za kuanzia.
“Hiki ni kikao muhimu sana, tunahitaji kurudisha heshima ya Morogoro katika Sanaa na Michezo, tunaamini Morogoro ina vipaji vingi sana na asilimia kubwa ya wachezaji wametoka Morogoro , tulikuwa na timu nzuri sana lakini leo tumebakiwa na timu moja Mtibwa Sugar lazima tujiulize ni wapi tumekosea ili tuanze na hapo, tunaamini tukishirikiana kwa pamoja Morogoro ya Viwango inawezekana”” Amesema DC Msulwa.
Mwisho. Amechukua nafasi ya kuwakaribisha wanamichezo wote , Wananchi, Vikundi vya Michezo ikiwamo jogging, Watumishi wa Umma na binafsi katika Mkutano wa kujadili changamotoz a Wanamichezo na Wasanii ambapo kabla ya mkutano huo kutakua na mbio fupi zitakazooongozwa na Jogging kuanzia mishale ya saa 12:30 asubuhi kwenye Viwnaja vya Shule ya Msingi Mwere hadi Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Jamhuri ambapo Mkutano huo utafanyika .
Kwa upande wa Msanii wa filamu na maigizo , Haviti Makoti, amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Morogoro huku akisema mpango aliouanzisha unalenga kuwajengea uwezo wasanii pamoja na Wananmichezo ili kutengeneza ajira kupitia tasnia ya filamu na michezo kwa ujumla.
Aidha, Makoti, amesema kuwa Wasanii wengi wa filamu Morogoro wamekuwa wakicheza filamu zao nje ya Morogoro na kwenda Jijini Dar Es Salaam, kutokana na Morogoro kuwa na shida ya kukuza vipaji vya sanaa jambo ambalo limekuwa likidumaza sanaa za waigizaji hao kutofikia malengo.
Hivyo, kwa niaba ya wasanii wenzake ,wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuwaongezea nguvu ikiwamo kutafuta wadau ili waweze kusaidiwa kazi zao za sanaa katika kukuza vipaji na kujipatia kipato kama njia moja wapo ya ajira na kujikomboa na umasikini.
Kwa upande wa mchangiaji , Kitutu Mshana, ameshauri kuwepo na Makongamano ya kimichezo na sanaa ambayo yatawajumuisha Wanamichezo wote wanaotokea Morogoro pamoja na wasaanii ili fedha zinazopatikana ziende kusaidia kuchangia huduma shuleni ikiwamo vitabu na madawati n.k.
Kitutu ,amesema ili michezo iwe endelevu haipaswi ikawa siku moja pekee ipo haja ya watumishi kukutani mishale ya jioni kufanya mazoezi ambapo kupitia wao wanaweza kukutana na kujadili masuala mbalimbali ikiwamo kuanzisha michango mbalimbali itakayoweza kusaidia kunyanyua michezo na sanaa katika Wilaya ya Morogoro.
Naye msanii Mwasity Juma, amemuomba Mkuu wa Wilaya kuweza kusapati michezo hususani katika suala zima la mitaji kwani wana uwezo wa kuandaa mipango mizuri ya kisanii kama matamasha lakini changamoto inakuwa ni ukosefu wa fedha za kutangaza matamasha hayo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa