Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebeca Nsemwa ameongoza mamia ya wadau waMazingira Manispaa ya Morogoro kupanda miti 3000 katika maadhimisho ya Wiki yaMazingira Duniani Manispaa ya Morogoro.
Zoezi la upandaji wa miti hiyo ikiwemo miti ya matunda na mikarafuulimefanyika Juni 04/2024 Shule ya Sekondari Konga Kata ya Mzinga.
DC Nsemwa, amesema kampeni yake ya sasa ni kuhakikisha Shule zote za Wilayaya Morogoro zinapanda miche ya mikarafuu isiyopungua 100.
" Tumepanda miti 3000, lakini maelekezo ya Mkoa wetu kipaumbele Chakwanza kupanda miti ya mikarafuu, na hapa tumepanda miti 2000 ya matundana tumegawa miti 1000 ya mikarafuu kwa Wananchi wa Luhungo,Mzinga na Milimani,tunataka mikarafuu hii iwe sehemu ya kuongeza vipato vyetu baada ya miaka 3,hata michango ya Wazazi ya chakula shuleni kama mikarafuu ikizaa tutapata fedhana shida zote za kuwabana Wazazi fedha ya chakula hazitakuwepo" Amesema DCNsemwa.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amempongezaDC Nsemwa kwa mapambano yake ya kuitaka Morogoro kuwa ya kijani lakinikusimamia Mazingira kikamilifu kwa kupanda miti ili kukabiliana na Mabadilikoya tabianchi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mazingira, Mhe. Hamis Kilongo,amesema Manispaa ya Morogoro itaendelea kupanda miti na kutunza Mazingira Kwakushirikiana na wadau wa Mazingira na kusimamia kikamilifu sheria ndogo yaMazingira ya mwaka 2024 ili kuhakikisha Mji unakuwa safi na Salama.
Meneja NEMC Mkoa wa Morogoro, Abel Sembeka, amesema NEMCitaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Halmashauri zote Mkoa wa Morogoro ilikuhakikisha uhifadhi wa Mazingira unakuwa kipaumbele kwa Wananchi.
Miongoni mwa wadau wa Mazingira, kutoka Benki ya Diamond Trust Bank (DTB Bank) , Meneja wa Masoko DTB Benki , Silvester Bahati , amesema DTBBenki wataendelea kusaidia shughuli zote za uhifadhi wa Mazingira kadriwatakavyoweza kijadiliwa kupitia Bajeti zao na kuwa Benki namba moja ambayoitakuwa mstari wa mbele kuchochea uhifadhi wa Mazingira nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Dkt. Maneno Matawa, amewashukuruwadau wa Mazingira waliojitokeza huku akiomba ushirikiano huo uendeleee kwaniadhima ya Manispaa ya Morogoro ni kuwa Jiji na hawawezi kuwa Jiji kama Mji badoni mchafu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa