• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC NSEMWA AZINDUA MRADI WA KISIMA SHULE YA SEKONDARI TUBUYU WENYE THAMANI YA MILIONI 18.2 .

Posted on: May 26th, 2023

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebeca Nsemwa, amezindua mradi wa kisima wenye thamani ya Shilingi Milioni 18.2 mradi uliofadhiliwa na Shirika la Hope for Kids la nchini Uswisi na kusimamiwa na Shirika la Education Gauge for growth Tanzania (EGG) lenye makao yake makuu Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza katika uzinduzi huo, DC Nsemwa, ameutaka Uongozi wa shule kuhakikisha kutunza miradi ya maji na kuwa walinzi wazuri wa miundombinu hiyo ambayo wadau wamekuwa wakisaidia kwa ajili ya wanafunzi kupata huduma bora ya maji.

"Niwashukuru EGG Tanzania, kwa kushirikiana na Hope for Kids kutoka Uswisi, mradi huu utawasaidia sana wanafunzi wa shule hii ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiteseka na suala la upatikanaji maji,naomba mshirikiane kwa pamoja katika kuhakikisha kwamba kuna uwajibikaji katika matumizi sahihi ya maji na kuhifadhi mazingira " Amesema DC Nsemwa.

DC Nsemwa, amezipongeza baadhi ya shule mbalimbali ambazo zimekuwa mstari wa mbele kutunza huduma ya miradi ya maji ikiwemo shule ya sekondari Sumaye, Tushikamane, Nanenane kwa usafi na utunzaji bora wa miundombinu ya miradi hiyo ya maji.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro na Afisa Elimu Sekondari, Gabriel Paulo, amesema Manispaa ya Morogoro itaendelea kutambua michango ya wadau wa maendeleo huku akitoa pongezi kubwa kwa EGG Tanzania na washirika wake Hope for Kids kwa kusaidia shule za Manispaa uchimbaji wa Visima.

"Nawashukuru sana EGG Tanzania jambo ni kubwa mmelifanya, niombe nina visima 15 katika shule zangu za Sekondari na nina uhaba wa visima 14 , ikiwapendeza katika miradi yenu inayoendelea niombe mnipatie visma vyengine maana bado taaasisi zetu za elimu maji ni changamoto" Amesema Gabriel.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa EGG Tanzania, Jumanne Mpinga, ameishukuru Serikali kwa kutoa fursa kwa asasi za kiraia kushiriki moja kwa moja katika kusaidiana na Serikali kwenye utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi ikiwemo elimu ambayo ndio msingi mkuu wa maendeleo ya jamii yoyote ile.

"Mkuu wa Wilaya mradi huu umefanikiwa kupitia jitihada za pamoja kati ya Serikali yetu, washirika wa maendeleo wa Hope for Kids kutoka nchi ya Uswisi, na wananchi wa Morogoro kwa ujumla, tunaamini kuwa miradi hii itakuwa na athari kubwa katika maisha ya wanafunzi wetu na jamii yote kwa ujumla" Amesema Mpinga.

Mpinga, amesema EGG Tanzania linaendesha mradi wa "maji safi na salama shuleni" (School Clean and safe water project ) nchini ambapo mradi huo umegawanyika katika sehemu tatu ikiwemo miradi midogo ya pampu za kusukuma kwa mkono au ( hand pump project ), miradi ya saizi ya kati ambayo miradi yake huwekwa miundombinu ya mnara na tanki la maji ambapo unabeba koki zisizo pungua 9 hadi 10 za kutoa maji huwekwa katika kuta za mnara kama mradi wa maji Tubuyu pamoja na miradi mikubwa ambayo inahusisha kuchimba na kujenga miundombinu ya usamabazaji wa maji katika kila kitongoji cha kijiji au Mitaa.

Aidha , ameishukuru timu ya wataalamu waliofanya utafiti. timu ya wahandisi wa EGG Tanzania waliosimamia uchimbaji na ujenzi, na timu nzima ya wafanyakazi wa EGG Tanzania ,Bodi ya Shule , wazazi , Mkuu wa shule ya sekondari Tubuyu, waalimu na wanafunzi kwa ujumla waliojitolea katika namna mbalimbali kuona mradi huo unafanikiwa.

Mwenyekiti wa Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Salum Kipira,ameipongeza Asasi ya EGG Tanzania na kusema kuwa wamekuwa msaada mkubwa hususani katika kutatua changamoto za kijamii haswa katika utekelezaji wa miradi ya maji shuleni.

Naye Diwani wa Kata ya Tungi, Mhe. Namala Mchunguzi, ameishukuru EGG Tanzania,kwa kuwakumbuka wanafunzi wa shule hiyo ambao walikuwa hawana huduma hiyo ya maji muda mrefu jambo amablo lilikuwa likipelekea kutembea umbali wa muda mrefu kutafuta maji na wengine kuwa watoro wanapopata nafasi ya kutoka nje ya shule.

Mwakilishi wa Diwani Kata ya Boma na Mtendaji wa Kata hiyo, Prisca Mawala,ameishukuru EGG Tanzania kwa msaada huo wa kisima huku akiushukuru Uongozi wa Tungi chini ya Diwani wake kwa kuilea vyema shule hiyo licha ya shule hiyo kuwa chini ya Kata ya Boma.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa