KAMATI ndogo ya afya Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Aisha Kitime, imefanya ziara ya kukagua miradi ya afya inayotekelezwa katika Manispaa na kutoa pongezi za uendeshaji wa miradi kwa kuzingatia viwango ikiwemo ubora wa majengo pamoja na kasi ya uendeshaji.
Kauli hiyo ameitoa Januari 19/2023 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya afya ikiwamo Zahanati na Vituo vya afya katika kuona huduma zinazozotolewa kwa wananchi.
Mhe. Kitime,amesisitiza muda uliopangwa wa uendeshaji wa miradi kukamilika uendelee kuzingatiwa na katika maeneo ambayo yameonekana kuna changamoto yafanyiwe kazi pamoja na kuboresha huduma za afya katika vituo hivyo.
"Tumetembelea miradi yetu ya afya, lengo la kamati hii ndogo ni kusaidia kamati kuu ya afya kufanya kazi kwa urahisi, ,tumeona ubora wa majengo ni mazuri na wauguzi wetu wanajitahidi kuwahudumia wagonjwa, kikubwa niombe kuwasisitiza waganga wafawidhi katika Vituo kuwashirikisha viongozi wenu wa ngazi ya kata kwenye Kila hatua kuepusha kutokea kwa changamoto mwishoni" Amesema Mhe. Kitime.
Mhe. Kitime, amewataka Waganga wafawidhi kuhakikisha katika vituo vyao kuna vifaa tiba vidogovidogo huku wakiendelea kusubiria vifaa vyengine vya huduma.
Mwisho wajumbe waliendelea kusisitiza katika changamoto zilizopatikana kwenye baadhi ya miradi kutiliwa mkazo kuhakikisha zinafanyiwa kazi ikiwa ni moja ya kazi ya kutimiza majukumu ya kamati.
Miradi iliyotembelewa na kamati ndogo ya afya ni Zahanati ya Kauzeni, Zahanati ya Konga Kata ya Mzinga, Zahanati ya Kata ya Kihonda, Zahanati ya Kata ya Chamwino pamoja na Zahanati ya Kata ya Lukobe.
Manispaa ya Morogoro kupitia mapato yake ya ndani imeshatekeleza ujenzi wa Zahanati 6 ikiwamo Mbuyuni, Kihonda Maghorofani, Sultan Area, Tungi, Mgaza Mindu, na Kiwanja cha ndege huku Zahanati nyengine zikiendelea na ujenzi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa