KAMATI ndogo ya afya Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe.Samwel Msuya imefanya ziara ya kukagua miradi ya afya inayotekelezwa katika Manispaa na kutoa pongezi za uendeshaji wa miradi kwa kuzingatia viwango ikiwemo ubora wa majengo pamoja na kasi ya uendeshaji.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Oktoba 15-2024 kwa niaba ya kamati, Mhe. Samwel Msuya, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya afya ikiwamo Zahanati ya Kata ya Mji Mpya ambayo kuna ujenzi wa wodi ya wazazi unaoendelea pamoja na Zahanati ya Mwembesongo ambayo imetengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio eneo la wodi ya wazazi.
Mhe.Msuya, amesisitiza muda uliopangwa wa uendeshaji wa miradi kukamilika uendelee kuzingatiwa na katika maeneo ambayo yameonekana kuna changamoto yafanyiwe kazi pamoja na kuboresha huduma za afya katika vituo hivyo.
"Tumetembelea miradi yetu ya afya, lengo la kamati hii ndogo ni kusaidia kamati kuu ya afya kufanya kazi kwa urahisi, ,tumeona ubora wa majengo ni mazuri na wauguzi wetu wanajitahidi kuwahudumia wagonjwa, kikubwa niombe kuwasisitiza waganga wafawidhi katika Vituo kuwashirikisha viongozi wenu wa ngazi ya kata kwenye Kila hatua kuepusha kutokea kwa changamoto mwishoni" Amesema Mhe. Msuya.
Mwisho wajumbe waliendelea kusisitiza katika changamoto zilizopatikana kwenye baadhi ya miradi kutiliwa mkazo kuhakikisha zinafanyiwa kazi ikiwa ni moja ya kazi ya kutimiza majukumu ya kamati.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa