Kamati ya Fedha na Uongozi Manispaa ya Morogoro imeridhishwa na kupongeza hatua ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo huku ikisisitiza miradi ambayo haijamalizka ikamilike kwa wakati ili iendelee kuwanufaisha Wananchi.
Hayo yamejiri Machi 17/2021 wakati Kamati hiyo ikifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu , Mhe. Pascal kihanga, walijionea hatua za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Ujirani iliyopo Kata ya Mkundi, Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari iliyopo Kata ya Mkundi yenye vyumba 6 ambavyo kati madarasa hayo, vyumba 3 vimejengwa kwa nguvu ya Wananchi na vyumba 3 kupitia ufadhili wa Diwani wa Kata ya Mkundi Mhe. Seif Chomoka.
Aidha, kamati hiyo , mbali na kutembelea miradi ya shule lakini walitembelea mradi wa Jengo la Wanawake Wajasiriamali Wasindikaji wa vyakula mbalimbali lililopo Kata ya Kihonda Maghofani, Maabara Kituo cha afya cha Mafiga, Ujenzi wa shule mpya ya Ghorofa ya Sekondari Kata ya Boma pamoja na kutembelea jengo la kitega uchumi DDC .
Kamati hiyo, imesema kukamilika kwa miundombinu ya shule kutasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na hivyo kutekeleza kwa ufanisi sera ya elimu bila malipo.
Pia imesema katika miradi hiyo ipo miradi ambayo itapelekea kuchangia ongezeko la pato la ndani ikiwemo mradi wa kitega uchumi wa DDC .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa