KAMATI ya Huduma za Uchumi, Elimu na Afya Manispaa ya Morogoroikiongozwa na Mwenyekiti wake , ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kingo, Mhe.Amini Tunda, pamoja na timu ya wataalamu ya Wakuu wa Idara na Vitengo imeeleza kuridhishwa na ubora wamiradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika hatua tofauti tofautikatika Manispaa ya Morogoro.
Wajumbewa Kamati hii wameeleza haya Julai 22-2024 katika ziara ya kutembelea nakukagua miradi ya maendeleo katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha2023/2024.
Katikaziara hii, Wajumbe wametembelea na kukagua ujenzi wa madarasa mapya shule yaSekondari Kingo pamoja na Shule ya Sekondari Nanenane, Hospitali ya Manispaa yaMorogoro , Zahanati ya Mji Mkuu pamoja na maboma ya madarasa Shule ya MsingiMisufini B Kata ya Mafiga.
Aidha,pamoja na kuridhishwa na ubora wa miradi hii ambayo kimsingi ipo katika hatuatofauti tofauti ya utekelezaji na mingine kuanza kutumika kutoa huduma ,wajumbe wameshauri ujenzi wowote ambao bado haujakamilika ukamilike kwa wakatiili utoa huduma kwa wananchi.
Akizungumzakwa niaba ya Kamati hiyo, Mhe. Tunda, ameishukuru sana Serikali ya awamu yasita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa kuendelea kuipatia fedha za miradi ya maendeleo Manispaa yaMorogoro.
Ujenzi wa madarasa matatu Shule ya Sekondari Kingo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa