NAIBU waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea Mathew amesema hatua inayofuata sasa kuhusu anwani za makazi na Posti Kodi ni kwamba kila mwananchi anatakiwa kuwa na anwani za makazi na kwa wafanyabiashara hicho kitakuwa ni moja ya vigezo muhimu katika kutoa leseni zao za biashara.
“Wafanya biashara wote watakapokwenda kuomba leseni ya kufanya biashara, ni lazima atoe anwani yake ya makazi, asipokuwa na anwani ya makazi hataweza kusajiliwa biashara yake” amesema Naibu Waziri Kundo.
Waziri Kundo amesema hayo Mei 18/2022 ,wakati wa uzinduzi wa uwekaji wa vibao vya anwani za makazi katika Kata ya Kichangani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro alipofanya ziara ya siku moja.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa