Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameambatana na , Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita , Mamea wa Halmashauri na Madiwani wamefanya ziara mkoani Morogoro katika Manispaa kuangalia kituo kipya cha mabasi Msamvu ili kujifunza namna ilivyofanikiwa kuweka mazingira mazuri kwa makundi yote wakiwemo wafanyabiashara na wasafiri
RC Makonda amesema Dar es salaam ipo katika hatua ya ujenzi wa stand Mpya ya kisasa itakayojengwa katika eneo la Mbezi Luis itakayogharimu zaidi ya shilingi billion 50.9 ambayo itakuwa na ukubwa Mara nne ya Stand ya Msamvu ambapo itakuwa na uwezo wa kupokea Mabasi 500 kwa wakati mmoja.
Aidha RC Makonda amesema Stand mpya ya Mbezi Luis itakuwa na Jengo la Abiria,Utawala, maegesho ya mabasi, shopping mall, Hotel,eneo la kupaki Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo,kituo cha polis na sehemu ya kuhifadhi mizigo.
Pamoja na hayo RC Makonda ameonyesha kufurahishwa na jinsi stendi ya Msamvu ilivyoweza kuweka utaratibu mzuri na kuzuia mianya ya wizi kiasi cha kuongeza mapato kutoka shilingi 350,000 hadi kufikia Shilingi Million 4.5 kwa Siku .
Kwa upande wa viongozi wa Mkoa wa Morogoro wameshukuru kupokea ugeni huo mzito na kuhahidi kutembelea jiji la Dar es salaam kujifunza mambo mengi ambayo Jiji hilo limepiga hatua na kupata sifa kubwa ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa