KAMISAA wa Sensa , na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Anna Makinda, amewataka Watanzania watambue umuhimu wazoezi la Sensa na kuanza kujiandaa kwa kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Hayo ameyasema Septemba 01/2021 katika Mkutano wa Sensa ya Majaribio iliyofanyika Mtaa wa Mtawala Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mhe. Makinda, amesema Sensa ya Majaribio ni moja ya mpango ambao Serikali imeuweka ili kuona jinsi Sensa ya itakaofanyika Mwaka 2022 itakavyoweza kufanyika na kufanikiwa huku akiwaomba watanzania watambue umuhimu wa zoezi hili kuanzia sasa na wajiandae kwa kuhesabiwa kwaajili ya maendeleo ya Taifa.
" Lengo la sensa ya watu na makazi ni kuiwezesha serikali na jamii kwa ujumla kuweka misingi ya kutunga sera ambazo zinatafanikisha maendeleo kwa Taifa na watu wake, hivyo ni vyema Wananchi wakalichukulia suala hili kwa uzito na umuhimu mkubwa , tunaamini Sensa ya Mwaka huu kuna mabadiliko makubwa yatatokea kikubwa ni ushirikiano wa Wananchi " Amesema Mama Makinda.
Mama Makinda amesema kuwa , mara baada ya kukamilika kwa sensa ya majaribio wanatarajia kukutana na wadau mbalimbali kwa ajili kujadili changamoto zilizojitokeza na kuboresha kwaajili ya sensa ya mwakani.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa, amesema kuwa kutoka na na umuhimu wa sensa ya watu na makazi Ofisi yake imedhamiria kuboresha zoezi hilo la Sensa ya majaribio ili kuweza kurekebisha kasoro zinazoweza kujitokeza hapo baadae.
Dk. Chuwa ,amesema kuwa katika sensa ya majaribio jumla ya kaya 5000 zitahojiwa kwaajili ya kupata taarifa zao muhimu ambazo zitaingizwa katika kumbukumbu za National Bureau of statistics (NBS).
Hata hivyo, Dk Chuwa, amesema kutokana na hali hiyo NBS itatoa mafunzo kwa watu wapatao 100,000 kwa ajili ya kukusanya taarifa kwa namna itakayo kidhi vigezo na mfumo thabiti wa mafunzo kwa watalaamu wake.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amesema kwa kutambua umuhimu wa sensa serikali imejipanga kikamilifu ili kuhakikisha sensa ya watu na makazi inafanikiwa kwa ubora wa hali ya juu ili kwenda sambamba na mafanikio ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Naye Mstahiki Meya amesema kuwa akiwa kama mwakilishi wa Madiwani wa Manispaa ya Morogoro, atashirikiana vyema na wananchi na kutoa ushirikiano wa kuwezesha zoezi la Sensa linafanikiwa, tunatambua umuhimu wa Sensa kwani hata sisi katika Bajeti zetu tukiwa na takwimu sahihi itatusaidia kuweka vipaumbele vyetu kwa wananchi wetu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa