Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw .Clifford Tandale ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2015/2016,na kusisitiza uongozi kufanya kazi kwa weredi na kuzingatia miongozo mbalimbali ya Serikali,hali itakayosaidia kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Clifford Tandale ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za hesabu kwa mwaka wa fedha 2015/2016 lililofanyika mkoani hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,akiwepo Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo na Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu wa mkoa wa Morogoro Ndugu Peter Mabwanga.
Aidha Katibu Tawala amewataka wakuu wa idara wa Manispaa akiwepo Mweka Hazina Ndg.Mbwana Msangi ,kuhakikisha anawasilisha asilimia 20 kwenye kata kwa lengo la kufanya shughuli za miradi ya Maendeleo kwa wananchi.
Naye Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za serikali wa mkoa wa Morogoro ameeleza kuwa chachu pekee ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa ni kila kiongozi kufanya kazi katika misingi inayotakiwa sambamba na kuimarisha ushirikin kati yao.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa