• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YAZINDUA KAMPENI YA SOMA NA MTI MASHULENI, YAANZA NA SUA NA MBUYUNI KWA KUPANDA MITI 1000

Posted on: February 25th, 2022

MANISPAA ya Morogoro, imezindua kampeni kabambe ya upandaji miti katika shule huku ikibainisha kuwa wamepanga kupanda miti zaidi ya milioni 1 na laki 5 kupitia wanafunzi wa shule za msingi,sekondari, vyuo, maeneno ya makazi na pembezoni mwa vyanzo vya maji.

Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 25/2022 ukijumuisha Shule mbili za Sekondari ikiwamo Mbuyuni na SUA ambapo miche hiyo imefadhiliwa na Shirika la SAT wadau wakubwa wa maendeleo hususani katika utunzaji wa mazingira.

Akizindua Kampeni hiyo yenye kauli mbiu ya “Soma na mti” Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Samwel Subi, amesema lengo la kuzindua Kampeni hiyo Mashuleni ni kuhakikisha wanafunzi waone zoezi la upandaji miti ni sehemu ya maisha ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

" Tumezindua Kampeni hii katika Shule ya Sekondari Mbuyuni na SUA, tunawashukuru wadau wetu SAT kwa kutupatia miche 1000 ambayo tumeipanda leo, tunashukuru Viongozi wa Kata, vyama vya Siasa, wadau wote wa Mazingira , wananchi na wanafunzi, kampeni hii ili ifanikiwe tunataka kila mwanafunzi apande mti mmoja na huo mti atautunza hadi atakapomaliza shule, nitoe rai kwa Wananchi kampeni hii isiwe mashuleni bali kila mtu apande miti katika maeneo yao na kila Taasisi ipande miti ili tuweze kukabiliana na Tabia nchi" Amesema Subi.

Subi, amewaagiza maafisa afya na Mazingira ngazi ya Kata kuhakikisha wananchi wanafanikisha upandaji wa miti milioni 1 na laki 5 ambayo Manispaa ya Morogoro imejiwekea ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Aidha, Subi, amewaagiza Maafisa Afya na Mazingira ngazi za Kata kuisimamia kampeni hiyo kwa kwenda mashuleni na vyuoni kuikagua miti hiyo ambayo itakuwa imepandwa.

Mwisho, Subbi, ameagiza kufufuliwa kwa Klabu za utunzaji wa mazingira katika shule pamoja na Maafisa elimu kuisimamia kwa vitendo kampeni ya soma na mti kuhakikisha inatekelezwa kikamilifu.

Naye , Balozi wa Mazingira  kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Mwakilishi wa Moro Kwanza Mazingira, Chage, amesema ukosefu wa mvua unasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kuna wajibu wa kuhakikisha mazingira yanatunzwa ikiwa ni pamoja na miti kupandwa.

Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Mhe. Samwel Msuya, ameishukuru Manispaa na wadau kuzindua Kampeni hiyo katika Kata yake , huku akiwataka wale wenye viwanja vipya kupanda miti mitatu katika viwanja hivyo ikiwemo wa kivuli na mti mmoja miwili ya matunda huku akidai kwamba agenda ya utunzaji wa mazingira katika Kata ya Mbuyuni iwe endelevu.

Naye,mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Elizabeth Ngonyani, ameiomba jamii na wanafunzi kusimamia kampeni hiyo ili ifanikiwe huku akiiomba serikali kuwachimbia kisima ili kurahisisha upatikanaji wa maji ya kutunza miti inayopandwa.

Shule ya Mbuyuni ni shule ya kwanza ambayo itaanzishwa shamba la Vitalu vya miche ya miti ya vivuli na matunda ikiwamo na maua ili kuwa mfano kwa shule nyingine lengo likiwa ni kuzalisha miche zaidi katika kusaidia kampeni hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa