• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA , WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA ULINZI KWA WATOTO

Posted on: June 16th, 2023

MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA, WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA ULINZI KWA WATOTO

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Pascal Kihanga, amewataka wazazi kuwa walinzi wa watoto ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia kwenye jamii.

Rai hiyo ameitoa Juni 16/2023 katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Morogoro iliyofanyika viwanja vya shule ya Msingi Mwembesongo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Kihanga, amesema kuwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ukatili kwa watoto bado vinaongezeka miongoni mwa jamii kila siku.

"Siku ya leo tukiwa tunaadhimisha Mtoto wa Afrika ni wazi kuwa tunalenga kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa na kutekelezwa katika nyanja zote ili watoto waweze kuwa na ustawi mzuri na kufikia malengo na ndoto zao za kimaisha" Amesema Kihanga.

Kuna Aidha,Mhe. Kihanga, amewataka wazazi kuweka mazingira Salama dhidi ya matumizi ya vifaa vya kielektroniki vikiwemo simu, kompyuta, runinga, radio, na mitandao ya kijamii ikiwemo whats up, twitter na facebook wakati watoto wanapokuwa wanavitumia.

Kuhusu unyanyaswaji wa kijinsia, Mhe. Kihanga, amesema bado wanawake wengi wananyamaza wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia na sababu kubwa ni kutokuwa na elimu ya kutosha na hivyo ushindwa kuripoti.

Mwisho, Mh. Kihanga, amepongeza Bunge la watoto huku akisema , kazi kubwa ya Bunge la watoto ni kuendelea kutoa elimu kwa watoto na jamii ili kuwawezesha watoto na jamii kutetea haki za watoto na kuhamasisha utekelezaji na usimamizi wa haki hizo na kutoa taarifa sehemu husika pale zinapokiukwa.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Faraja Maduhu,amesema Manispaa ya Morogoro imeweza kuunda Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika kata 29.



Maduhu ,amesema kamati hizo zinafanya kazi ya kuelimisha jamii juu ya haki za msingi za Wanawake na Watoto pamoja na kuzilinda.

Kwa upande wa Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, David Max, amesema hali ya ukatili imekuwa ni changamoto huku akiomba jamii kulivalia njuga suala hilo.



Max, amesema mtu anapopata tatizo la kingono anapaswa kutopoteza ushahidi ili kuweza kuwa rahisi kushughulikia tatizo hilo.



" Matukio yanatokea lakini wapo wazazi wamekuwa wakificha kutoa taarifa au wanachelewa kutoa taarifa, niombe wazazi kutochelewa kutoa taarifa mara baada ya kujua tatizo limetokea ili kupata ushahidi mzito wa kuweza kumuunganisha na mtuhumiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria" Amesema Max.

Miongoni mwa shughuli ambazo Manispaa ilizifanya kuelekea maadhimisho hayo ni Kuandaa Bunge la Watoto la Manispaa, 1. Kuundwa upya mabaraza ya watoto kuanzia ngazi za mitaa, kata na Halmashauri ambapo hadi sasa jumla ya baraza 01 la Halmashauri limeundwa, kata 28 na mitaa 263, Kufanyika uchaguzi wa viongozi wa baraza la watoto la Manispaa, pamoja na 1. Kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia katika kata 10, shule 14 zikiwemo shule 08 za msingi, 01 ya chekechea na 5 za sekondari.

Kauli Mbiu ya siku ya Mtoto wa Afrika mwaka 2023 inasema “Zingatia Usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidijitali”. Kauli mbiu hii inaelekeza wazazi, walezi, wadau na serikali kuweka mazingira Salama na kuchukua tahadhari juu ya matumizi ya mitandao kwa watoto.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa