Katika kuboresha utendaji wa kazi wa Serikali, tarehe 09.03.2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa, maafisa tawala wa mikoa, wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART).
Katika mabadiliko hayo, rais Samia amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Bunda, ndugu Emmanuel J. Mkongo, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro.
Tarehe 11.03.2024 ndugu Mkongo aliripoti kwenye Ofisi ya Manispaa Morogoro tayari kwa kuanza majukumu yake.
Watumishi wa Manispaa ya Morogoro wanamshukuru sana aliyekuwa mkurugenzi wa Manispaa hiyo, ndugu Ally H. Machela kwa utendaji wa kazi mzuri kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya Manispaa ya Morogoro, na wanamtakia utendaji mwema zaidi katika majukumu yake mapya.
Pia, wanampongeza ndugu Emmanuel Mkongo kwa kuteuliwa kuja kuiongoza Manispaa ya Morogoro, na wanaahidi kushirikiana naye ili kuendelea kuiimarisha Manispaa na wananchi wake kwa ujumla.
MWISHO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa