MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka wanufaika 19 waliopatiwa mitaji kwa watu wenye Ualbino Manispaa ya Morogoro kuhakikisha wanatumia mitaji hiyo kwa kutekeleza malengo waliyojiwekea.
Kauli hiyo,ameitoa, Septemba 6/2022 wakati wa hafla fupi ya utoaji wa ruzuku kwa watu wenye Ualbino kupitia ufadhili wa ADRA Tanzania katika Ukumbi wa Mbaraka Mwinshehe Manispaa ya Morogoro.
‘’ Ninawaomba sana mitaji hii mliyopewa mkaitumie kwa malengo mliyojiwekea,kuna baadhi ya watu wanatabia wanapopewa mitaji au mikopo hii hubadiri mawazo na malengo yao na kuamua kuzigawana fedha kwa matumizi binafsi,kumbukeni wafadhili wetu wametoa matarajio yao ni kuona fedha hizi zinazaa matunda, lakini niwaombe mkajiunge vikundi Manispaa inatoa asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya ndani ya kila mwezi ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi, na njia nzuri ya ilionekana kupitia vikundi , Imani yangu mtafanya vizuri kwa kuwa tayari nimesikia mshapata mafuzo juu ya biashara zenu” Amesema Mhe. Kihanga.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa ADRA Tanzania, Sam Oyortey, amesema bado kuna kundi kubwa la watu wenye ulemavu wanaopaswa kuwezeshwa ujuzi na mitaji ili waweze kujitafutia kipato.
Oyortey, ameiomba Manispaa ya Morogoro licha ya walemavu hao kupatiwa mitaji lakini Manispaa ijikite katika kuona namna ya kuwaongezea mitaji katika mikopo yao ya asilimia 2.
Naye Mwenyekiti wa Watu wenye Ualbino Mkoa wa Morogoro, Hassan Mikazi, amesema kukosekana kwa mitaji kwa watu wenye ulemavu umesababisha wengi wao wanakosa fursa mbalimbali ambazo zingeweza kupunguza viwango vya umasikini.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa