• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MEYA KIHANGA AWATAKA WAZAZI KUCHANGIA CHAKULA CHA WATOTO WAKIWA SHULENI

Posted on: June 3rd, 2021

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka wazazi kuwa na desturi ya kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao mashuleni ili kuongeza kiwango cha ufaulu kwani watoto wengi wamekuwa wakifeli kutokana na utoro.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa hafla iliyoandaliwa na Uongozi wa Shule ya Msingi Mazimbu 'A' ya kuwasilisha taarifa ya shule hiyo kwa wazazi wa wanafunzi hao iliyofanyika Juni 3/2021 katika viwanja vya shule hiyo.



Mhe. Kihanga, amesema kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikizikabili shule nyingi ni kutokana na wazazi kutochangia fedha kwa ajili ya chakula cha mchana kwa watoto wao hali ambayo huchangia kuwepo kwa utoro kwa watoto ambao hawali chakula mashuleni.

Amesema kuwa kutokana na baadhi ya wazazi wengi kutokuwa na mwamko wa kuchangia chakula mashuleni, kumekuwa kukichangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kuwepo kwa ufaulu usioridhisha kwa wanafunzi , hivyo amewaomba wazazi husuani wa shule za Msingi na Sekondari kuweza kutoa ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya elimu ya watoto wao kwa kuchangia fedha kwa ajili ya chakula ili watoto waweze kusoma kwa utulivu.



"Kwa kweli uwepo wa baadhi ya wazazi wengi kutochangia chakula cha mchana kwa ajili ya watoto wao ndio wamekuwa wakichangia shule zetu kuweza kupata matokeo yasiyoridhisha, kwani wengi wa wanafunzi wanaopata ziro ni wale ambao hawali chakula cha mchana hapa shuleni, hivyo tunawaomba sana wazazi wachangie chakula cha watoto ili tuhakikishe tunafuta division ziro."Amesema Mhe. Kihanga .

Katika hatua nyingine, amechukua nafasi ya kuwapongeza Waalimu wa Shule za Msingi Mazimbu A na B kwa kufanikiwa kufaulisha wanafunzi kwa kila mwaka hususani katika upande wa shule za Serikali Manispaa ya Morogoro.

Aidha, amesema licha ya changamoto walizozitaja , atahakikisha kwa kushirikiana na Uongozi wa Shule zote 2, pamoja na wananchi wanaendeleza desturi ya kujenga darasa moja kwa kila mwaka ili kuondokana na changamoto za mrundikano wa wanafunzi katika darasa moja.



Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mazimbu A, Mwl. Anitha Nathan,amesema kuwa kuna mambo mengi yanayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika Shule zao za Msingi ikiwemo Wanafunzi kutokupata chakula cha mchana mashuleni hali inayowafanya watoto kutofuatilia masomo ipasavyo.



"Tumepokea wito kutoka kwa Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Morogoro , kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa la kuwataka wazazi kuchangia chakula cha mchana cha Wanafunzi, upande wetu tumeshawaita na kuwaeleza wazazi ili waweze kuchangia , lakini bado katika upande huu hatujaweza kufanikiwa sana , niwaombe sana wazazi waendelee kuchangia kwani tukichangia michango hii ya chakula itakuwa ni jambo ambalo litasaidia sana watoto wetu kuweza kusoma kwa umakini wakiwa wameshiba na wakaelewa vipindi darasani "Amesema Mwl. Nathan.

Aidha, amesema licha ya changamoto ya chakula lakini zipo changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto za uhaba wa matundu ya vyoo kwa wanafunzi wa kike na wakiume, mshahara kwa ajili ya mlinzi n.k.

Mbali na hafla hiyo ya wasilisho ya taarifa kwa wazazi juu ya mienendo ya shule hiyo ikiwamo changamoto , mafanikio pamoja na nini kifanyike, lakini wameendesha zoezi la kuwatunukia zawadi wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo tofautitofauti na kutambua vipaji vyao.

Mwisho, Mstahiki Meya , ameendesha zoezi la harambee la wazazi kuweza kuchangia walichonacho ili kuweza kuwatia moyo waalimu wanaopambana na wanafunzi shuleni katika kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa wanafunzi hao na kuinua viwango vya elimu ambapo mwisho wa harambee hiyo jumla ya shilingi 80,000/= ilipatikana kupitia michango ya wazazi walioguswa na harambee hiyo .

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa