• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MEYA MANISPAA MOROGORO ATAKA MIRADI IKAMILISHWE KWA WAKATI

Posted on: April 30th, 2020

Mstahiki Meya Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, ameitaka Miradi yote inayotekelezwa kwenye Manispaa ya Morogoro hususani miradi ya Soko Kuu la  Kisasa na Stendi mpya ya Daladala Mafiga imalizike kwa wakati.

 Hayo ameyasema Aprili 30,2020 kwenye Kikao cha Baraza la  Madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Kihanga , amesema wananchi wanasubiri miradi yao wamekaa muda mrefu kwenye maeneo ambayo siyo rasmi.

 " Tunaomba miradi hii ikamilike haraka, tumewavumilia sana wakandarasi, Manispaa yetu ni sikivu mno lakini ifike wakati tuseme inatosha, Masoko ambayo tumewaweka wafanyabiashara wetu siyo rafiki sana  ukizingatia kipindi hiki cha ugonjwa Wa Corona hata tunavyokwenda kuwahamasisha wasipange Vitu chini je  tunawapeleka wapi? Hata Stendi yetu imejaa kwa sasa Magari ni mengi mpaka yanasababisha msongamano wawatu na sisi hatutaki msongamano huo  , tunawaomba wakandarasi waharakishe ili ukifika muda tuliowapa watukabadhi miradi hiyo tuipeleke kwa wananchi " Amesema Kihanga.

 Aidha, Kihanga, ametaka taarifa ya matumizi ya   hela itakayobaki katika Ujenzi wa Stendi mpya ya Daladala Mafiga,baada ya kuwa wamepunguza baadhi ya vitu ili itumike kujenga vioski kitu ambacho ni hitaji la wananchi



Katika hatua  nyingine amelipongeza Baraza la  Madiwani    pamoja na Mkurugenzi Wa Manispaa, Sheilla Lukuba, kwa maamuzi ya kufufua upya ujenzi wa Stendi ya Kaloleni baada ya kupata Mkandarasi mpya Nandhra Engineering aliypewa Mkandarasi hiyo kwa muda muda wa miezi 2 sawa na siku 60.

Amesema huo ni uamuzi mzuri  kwani mradi huo  unakwenda kuongeza chanzo chengine cha Mapato na kuifanya Manispaa kutotegemea Fedha za Ruzuku kutoka Serikalini . .

Lakini kubwa amemtaka Mkandarasi aliyekabidhiwa Mradi huo kwenda na kasi inayotakiwa na kukamilisha ujenzi huo kwa wakati. " Nandhra Engineering tumewakabidhi mradi huu kwa vile tunafahamu uwezo wenu, msifanye ubabaishaji kama wenzenu, mlianza vizuri miradi yetu ya Soko na Stendi Mafiga na sasa hii ni fursa nyengine mmeipata itendeeni haki  ili muweze kupata tenda  nyengine ndani na nje ya Manispaa yetu" Ameongeza Kihanga.


Hata hivyo ameendelea kutoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kufuata ushauri wa Wataalamu wa Afya katika kujikinga na Ugonjwa wa Corona ikiwemo kunawa Maji tiririka na sabuni, kutumia Vitakasa mikono ( Sanitizer), pamoja na kuepuka msongamano isiyo ya lazima na kukaa nyumbani kama mtu  hana sababu ya Msingi ya kutoka


Mwisho amechukua nafasi ya kutoa pole kwa niaba ya Baraza la  Madiwani kufuatia kifo cha aliyekuwa Naibu Meya Manispaa Morogoro na Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mhe. Isihaka Sengo huku akiwataka Wanafamilia, Ndugu pamoja na Marafiki kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha mpito .


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa