MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, amepiga marufuku wakandarasi wasio na sifa kuomba kazi katika Manispaa ya Morogroro.
Hayo ameyasema leo Mei 5, 2020 mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa Ujenzi wa Stendi ya Daladala ya Kaloleni unaoendelea kufuatia Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kuvunja mkataba na Mkandarasi Kampuni ya Fast na kukabidhi mradi huo kwa mkandarasi mpya kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Nandhra.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Kihanga, amesema Wakandarasi wasio nasifa marufuku kuomba kazi Manispaa ya Morogoro na wakigundulika wamepatiwa kazi na wakashindwa kutekeleza kwa wakati watapata hasara zaidi ya kile walichokiomba.
“Leo nimeona nipite kuangalia ujenzi huu wa Stendi ya Kaloleni , wiki iliyopita katika Kikao cha Baraza Mkurugenzi wa Manispaa alitueleza kwamba washavunja mkataba na Mkandarasi wa zamani na wamekabidhi mradi huo kwa mkandarasi mpya ambaye ndiye anayeendelea na ujenzi wa Soko Kuu pamoja na Stendi Mpya ya Daladala, nimeona kazi za kusafisha zimeanza tofauti na ilivyokuwa mwanzo, matarajio yangu anaweza kwenda na muda kama tulivyoshauri kwenye Baraza, nafikiri ilitumika busara kumpa mkandarasi huyu mradi kwani muda uliobakia ni mdogo isingewezekana kuanza kutafuta mkandarasi mpya, Ombi langu kwa Mkandarasi tufanaye kazi na tumalize kwa wakati kwani fedha hizi tulizopewa kutoka ULGSP muda wake unakwisha Juni 30 mwaka huu 2020, ambapo tukishindwa fedha hizi zitarudi zilipotoka" Amesema Kihanga.
Aidha amemtaka Mkandarasi kwenda na wakati kwa kipindi hiki cha miezi miwili waliyopewa wahakikishe kwamba Stendi hiyo inaanza kutumika kwani waliwaondoa wananchi katika eneo hilo wakiwa na matumaini ya kupata Stendi mpya yenye ubora licha ya kutokea ukwamishaji uliojitokeza kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Fast.
Amesema matarajio yake mradi huo utamalizika vizuri ili Wananchi waliokuwa wakinufaika na huduma hiyo ya Stendi waweze kupata huduma kama kawaida yenye ubora kwa wasafiri na kuwa moja ya Chanzo chengine cha Mapao ya ndani katika Manispaa.
Hata hivyo amelaani vikali Wakandarasi wasio nasifa kupokea fedha za ujenzi wakati wakijua hawana uwezo wa kujenga huku akimuomba Mkurugenzi wa Manispaa kufuatilia ili kuhakikissha fedha zote ambazo Mkandarasi wa Fast alizichukua zinarudi.
“Kumekuwa na maswali mengi watu wakijuliza hususani hawa wenzetu wa daladala ambao tuliwahamisha eneo hili kupisha mradi lakini mategemeo yetu yalikuwa ni mazuri kukamilisha mradi huu kwa wakati , kwahiyo nalaani sana wakandarasi wanaomba kazi huku hawana uwezo, mbali na kupewa advance ya Shilingi Milioni 100 lakini bado walishindwa kufanya kazi , lakini ni wahahakikishie hizi ni pesa za Serikali zitarudi na sheria itafuata mkondo wake, namtaka Mkandarasi amalize kazi hii kwa wakati kama tulivyokubaliana katika Mkataba akichelewa mpaka ikafika mwezi wa 6, 2020 hizi fedha hazitakuwa za kwetu “ Ameongeza Kihanga.
Hata hivyo ameendelea kutoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kufuata ushauri wa Wataalamu wa Afya katika kujikinga na Ugonjwa wa Corona ikiwemo kunawa Maji tiririka na sabuni, kutumia Vitakasa mikono ( Sanitizer), pamoja na kuepuka msongamano isiyo ya lazima na kukaa nyumbani kama mtu hana sababu ya Msingi ya kutoka
Kwa upande wa Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Eng. Juma Gwisu, amesema kwa sasa Mkandarasi yupo site na baadhi ya Malighafi tayari yameashaanzawa kutengenezwa na ameshasafisha eneo kwahiyo anaimani kazi itafanyika vizuri .
“Kama unavyoona Mkandarasi wetu ameanza kwa kasi kubwa , Yule wanyuma tulishavunja makataba naye na sheria zote tulifuata, lakini katika Ujenzi huu tutajenga Choo cha kisasa ambacho kitazingatia watu wenye ulemavu lakini zaidi hata Ofisi ya Kata tutaiboresha ili iendande na ubora wa Stendi” Amesema Gwisu.
Gwisu amesema kuvunja mkataba na Mkandarasi wa Kampuni ya Fast kumetokana na Mkandarasi huyo kushindwa kufuata masharti ya mkataba wake ya kukamilisha Ujenzi wa mradi huo wa Ujenzi wa Stendi ya Daladala Kaloleni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa