• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MEYA MANISPAA YA MOROGORO AZINDUA MAGARI 2 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 110.

Posted on: July 9th, 2021

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amezindua magari 2 yenye thamani ya shilingi milioni 110 yaliyonunuliwa na Manispaa ya Morogoro kupitia mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2020/2021 .

Tukio hilo la uzinduzi wa magari hayo limefanyika leo Julai 9/2021 nje ya Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Mhe. Kihanga, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa ununuzi wa magari hayo ambayo yatasaidia sana katika ukusanyaji wa mapato kwakuwa Manispaa  imekuwa na uhaba wa magari ambayo yamekuwa nguzo muhimu ya kusafirisha watumishi katika maeneo ya kazi hususani ukusanyaji wa fedha.

Kihanga, amewataka Watumsihi Manispaa ya Morogoro kuyalinda magari hayo na kuyafanyia huduma mara kwa mara kila inapofika wakati wake ili yaendelee kutoa huduma.

" Mmefanya jambo zuri sana, tunaamini sasa tunakwenda kurahisisha kazi katika majukumu yetu, haya magari ni mapya kabisa yanahitaji sana huduma za mara kwa mara , msiyatumie mpaka mkayasusa na kuyatelekeza, gari ukilitelekeza sana linaongezeka ubovu, sasa sitarajii kuyaona yakiwa na hali mbaya maana mkifanya hivyo mtajikuta mmepoteza fedha bure " Amesema Kihanga.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, amesema gari hizo zimenunuliwa kwa kiasi cha shilini 110,984,860 ambapo kwa gari moja limegharimu kiasi cha shilingi 55,492,430 kupitia kwa wakala wa huduma za ununuzi Serikalini, GPSA.

Waluse amesema mara baada ya GPSA kukamilisha mchakato wa manunuzi ikiwemo kuyakagua na kuyasajili waliwakabidhi kwa ajili ya kuendelea na kazi iliyokusudiwa.

"Taratibu zote zimefuatwa kikamilifu katika ununuzi wa magari ikiwemo kupata kibali kutoka  Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma ambapo kila gari ina uwezo wa kubeba abiria 4 pamoja na dereva , tunaamini magari haya yatatusaidia sana katika shughuli zetu za maendeleo na tunaahidi kuyatunza na kuyafanyia huduma mara kwa mara " Amesema Waluse.

Manispaa ya Morogoro imenunua aina ya magari ya New Suzuki Jimmy yenye namba za usajili wa SM 13779 na SM 13780 yenye ukubwa wa injini (Engine Cpacity ) ya 1462 .

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa