• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MHANDISI NYAMUHANGA APONGEZA MANISPAA YA MOROGORO KWA KUKAMILISHA UJENZI SOKO KUU LA KISASA

Posted on: December 7th, 2020

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI , Mhandisi Joseph Nyamuhanga, ameonyesha kufurahishwa na ujenzi wa soko kuu la kisasa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika ujenzi ambao umekamilika kwa asilimia 100 ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 17.6.

Pongezi hizo, zimetolewa leo Desemba 07/2020, baada ya Eng.Nyamuhanga kufanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa Soko Kuu la Kisasa pamoja na kupitia taarifa ya mradi huo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kuona maeneo mbalimbali katika soko hilo , Eng. Nyamuhanga, amesema kuwa licha ya kuwepo na ujenzi wa miradi ya masoko katika Mikoa ya Mtwara, Dodoma, Njombe na Dar es Salaam , lakini amefurahishwa na Ujenzi wa Soko la Manispaa ya Morogoro ambapo Ujenzi wake umezingatia mahitaji ya wafanyabiasha wanataka nini katika soko hilo.

"Nampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha hizi, pia Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya , Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro na timu yake ya Wataalamu bila kumsahau Mhandisi aliyesimamia ujenzi huu,pamoja na watumishi wote wa Manispaa ya Morogoro kwa ushirikiano mliouonyesha katika utekelezaji wa mradi huu ,hii inaonyesha jinsi gani mlivyo makini katika usimamizi wa miradi,Manispaa ya leo siyo ya jana angalia sasa mna stendi ya Msamvu,mmejenga stendi ya daladala,haya ni mafanikio makubwa sana katika Serikali ya awamu ya tano"amesema Eng. Nyamuhanga.

“Lengo la miradi hii ya Kimkakati ni kwa ajili ya kukuza Miji na kuzijengea Halmashauri uwezo wa kujitegemea, lakini nawapongeza sana tunakata matokeo chanya kama haya yaendane na thamani ya fedha zinazotolewa ."Ameongeza Eng. Nyamuhanga.

Eng. Nyamuhanga , amesema kufuatia ombi la Manispaa  kutaka kutengeneza mitaro inayozunguka Soko, Ofisi ya TAMISEMI imepokea ombi hilo na wamekubali kutoa Shilingi Milioni 470 kwa jili ya kuanza mchakato wa ujenzi wa mitaro hiyo ili kuzuia maji kukaa wakati wa mvua.

“ Haiwezekani mradi mkubwa kama huu , ukazungukwa na maji wakati wa mvua, tumepokea maombi yenu , sasa tumekubali kuwapatia shilingi Milioni 470 , kwahiyo niwaombe TARURA Manispaa ya Morogoro waanze haraka sana mchakato wa kutangaza mdhabuni ili kazi hiyo ianze mara moja “ Ameongeza kwa msisitizo Eng. Nyamuhanga.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, ameipongeza Serikali kwa kuiingiza Barabara ya Kisaki katika mpango wa kuweka lami ambapo itarahisisha usafirishaji wa mazao kutoka Morogoro Vijijini kuja Soko Kuu.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema Soko hilo linatarajia kutoa ajira 2500 kwa Wananchi, ambapo ajira rasmi 2000 na zisizo rasmi 500.

Lukuba, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli, kwa kutoa fedha hizo kwani itasaidia sana Manispaa kupunguza kutegemea ruzuku kutoka Serikali Kuu ambapo kwa mwaka wanategemea kukusanya fedha zaidi ya Bilioni 3 katika Soko hilo na hii itafanya ongezeko la Shilingi Bilioni 11 kutoka Bilioni 8 za Bajeti kwa mwaka.

Aidha, amesema Soko hilo linatarajia kufunguliwa rasmi Desemba 15, 2020.

Akielezea kuhusu mradi huo, Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu, amesema ujenzi huo utakuwa na Maduka 304, Meza 900, maeneo makubwa 16 ya kupangishwa kwa mita za mraba (benki, maduka makubwa , ofisi nk) maegesho ya magari makubwa 5 ya mizigo kwa pamoja, maegesho ya magari madogo 143 kwa pamoja, vyoo, migahawa, stoo 36 za mitumba, bucha pamoja na eneo la kuchinjia kuku.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa