Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo amewakumbusha wenyeviti wa Mitaa wote wa Manispaa ya Morogoro kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.
Akizungumza katika kikao na wenyeviti hao kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ,Mkuu huyo wa Wilaya amesema ni wajibu wa kila mwenyekiti kuyatambua majukumu yake na kuyatekeleza.
Aidha aliainisha majukumu hayo ikiwa ni kuwa Mwenyekiti wa Mikutano yote ya kamati ya Mtaa,kusuluhisha migogoro midogomidogo ambayo haistahili kuitisha mkutano wa kamati ya mtaa,kuwaongoza na kuwahimiza wakazi wa mtaa kushiriki shughuli za Maendeleo,kuwakilisha mtaa kwenye kamati ya Maendeleo ya Kata,kusimamia utunzaji wa rejista ya wakazi wa Mtaa, kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa watu na mali zao.Pia kusimamia na kuhamasisha ulipaji wa kodi na ushuru mbalimbali.
Nao wenyeviti wa mitaa wametoa shukrani na pongezi kwa Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuamua kuitisha kikao na kuzungumza nao na kukumbushana utekelezaji wa majukumu mbalimbali na wao kuweza kutoa kero zao.Aidha wameomba mikutano kama hiyo iwe ni endelevu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa