• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MHE. MABULA APIGA MARUFUKU UJENZI WA MAENEO YA WAZI YA SERIKALI

Posted on: July 13th, 2021

Naibu Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angeline Mabula, amepiga marufuku ujenzi katika maeneo ya wazi yote huku akiwatahadharisha wanaofanya hivyo.

Kauli hiyo ameitoa Julai 13/2021 kwenye eneo la Stendi ya Daladala Mafiga Manispaa ya Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku 2 ya kusikiliza na kutatua kero za migogoro ya ardhi Mkoa wa Morogoro.

Kauli ya waziri imekuja kutokana na kukithiri kwa watu kufanya ujenzi maeneo ya wazi na wamekuwa wakidai kuwa na vibali vya Manispaa.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara, Mhe. Mabula,amesema kuwa kumeibuka wimbi la wananchi ambao wamekuwa wakienda kinyume na sheria za mipango miji ya kujenga nyumba katika maeneo ya wazi.

Mhe. Mabula ,amesema kuwa sheria itachukua mkondo wake dhidi ya wote ambao watakaidi na kufanya ujenzi kwenye maeneo hayo.

"Lengo la kuja hapa kuongea na nyinyi leo ni kusikiliza na kutatua kero za migogoro ya ardhi pamoja na kuangalia wale ambao wamekuwa wakijenga katika maeneo ya wazi ya Serikali, kumbukeni hayo maeneo ya wazi Serikali imeyatenga kwa kazi maalumu, sasa unapojenga hapo unajitafutia mgogoro ambapo mwisho wa siku huna chako, acheni mara moja hiyo tabia lengo la Serikali sio kumnyanyasa mwananchi lazima muyaheshimu hayo maeneo" Amesema Mhe. Mabula.

Aidha, amesema migogoro mingi imekuwa ikisababishwa na viongozi kuanzia ngazi ya Vitongoji hadi Manispaa.

"Wapo viongozi wanaochukua maeneo ambapo wanasababisha changamoto zisizo na sababu, niwaombe watumishi wa Halmashauri zote nchini , popote nitakapo kuta kuna kesi ya kiongozi na mtu wa kawaida na mtu wa kawaida umemkuta pale basi tutaomba hati hiyo ifutwe na kubadilishwa kwa sababu kesi zinakuwa ni nyingi ukiangalia watumishi wamehusika na zaidi ni mtu mwenye madaraka , hatupingani na maamuzi ya Mahakama, tunachosema ni taratibu za utendaji kazi ndani ya Ofisi za Serikali,tusingependa kesi za namna hiyo zijirudie" Ameongeza Mhe. Mabula.

Katika hatua nyingine, amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kwa kushirikiana na Watendaji ngazi ya Kata kuhakikisha wanakuwa na majukumu ya kuangalia ujenzi holela unaofanywa katika maeneo yao na kuweza kudhibiti .

"Yoyote anayejenga katika eneo liwe limepimwa au halijapimwa akuonyeshe kibali, maeneo yote yameshatangazwa kuwa ni maeneo ya mji, haiwezekani mtu ajenge kama yupo kwenye kijiji , Wakurugenzi mkikuta maeneo nyumba zimeshamiri bila mpangilio ,angalieni namna ya kuwashughulikia watendaji wenu wa Kata kwani ujenzi bila vibali ni chanzo cha ujenzi holela" Amesisitizia Mhe. Mabula.

Kwa upande wa Kamishina Msaidizi wa ardhi Mkoa wa Morogoro, Frank Minzikutwe, amesema ujenzi holela na uvamizi wa maeneo vimekuwa vyanzo vikubwa vya kuzalisha migogoro katika maeneo mengi jambo ambalo linapaswa ushirikiano mkubwa wa kuweza kudhibiti matukio kama hayo.

"Tutaanza kuwa wakali sana katika ujenzi holela, hali sio shwari kabisa, mnatudharirisha watendaji wenu tunaonekana hatufanyi kazi, mkianza kujenga kiholela hadi milimani unafikiri hata hayo maji tunayoyategemea kutoka Mindu hatutayapata, uchafu kwenye bwawa hautapungua, niwasihi sana ndugu zangu acheni ujenzi holela na tutapita kuangalia maeneo hayo na wale wanaofanya hivyo tutachukua maamuzi magumu" Amesema Minzikutwe.

Aidha, Minzikutwe, ameelezea eneo la kichangani ambalo Serikali imelitenga  kwaajili ya  Reli na  kuwataka wananchi wanaofanya shughuli za kilimo katika eneo hilo kutambua mali hiyo sio yao na watambue walihifadhiwa mpaka Serikali itakapo taka kutumia eneo hilo na amewaelekeza viongozi wa Reli kusimamisha shughuli za kilimo katika eneo hilo kazi yao iwe ni kufyeka , kwani watu wakisaidiwa wanajiona kama ni wamiliki.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa