MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amewaagiza Wataalamu wafya pamoja na watumishi kutoa vipaumbele kwa Wazee wanapofuata huduma katika Ofisi zao.
Kauli hiyo, ameitoa leo Oktoba 1,2021 ikiwa ni Siku ya Wazee Duniani ambapo kila mwaka Wazee wamekuwa wakienzi siku hii.
Akizungumza juu ya Siku ya Wazee Duniani, Machela, ametaka sehemu zote zinazotoa huduma kutenga madirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wazee ili kuwaondolea usumbufu wa kupanga foleni.
"Wazee wetu ni hazina, uzee haukwepeki, kila mtu hapa ni mzee mtarajiwa hivyo, kuna kila haja ya kuwatengea Wazee hawa madirisha ya kupata huduma ili Wazee hawa wasiweze kupanga foleni ndefu wanapokwenda kupata huduma kwenye ofisi hizo"Amesema Machela.
Amesema , wazee ni kundi linalohitaji kuhudumiwa haraka mahali popote wanapokwenda badala ya kuendelea kunyanyaswa kwa kupanga foleni kama watu wa makundi mengine.
Aidha, Machela, ameziomba ofisi zote za Serikali zilizopo Manispaa ya Morogoro kuhakikisha zinatoa huduma kwanza kwa wazee ili wasiendelee kukaa sehemu hizo.
Katika hatua nyingine, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro , Dr Charles Mkombachepe, amesema wazee wanatakiwa kupewa huduma ya haraka popote wanapokwenda.
“Wizara ya Afya ilishaagiza mzee ahudumiwe kwanza anapokwenda kupewa huduma kwenye hospitali zetu, nasisitiza hili kwamba wazee wetu wanatakiwa kuthaminiwa,” Amesema Dr. Mkombachepe .
Dr. Mkombachepe , amesema kwa sasa bado wanaendelea na zoezi la kugawa Vitambulisho vya msamaha wa Matibabu bure.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa