• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO AWALIMA FAINI WALIOKIUKA BEI ELEKEZI YA VITAKASA MIKONO VYA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA

Posted on: March 24th, 2020

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewapiga faini na kuvifungia vituo vinavyouza bei ya vitakasa mikono kwa gharama kubwa tofauti na bei elekezi ya Serikali.

Hayo yamejiri leo Machi 24, 2020, kufuatia agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka wale wote wanaouza vitakasa mikono tofauti na bei elekezi kushughulikiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Sheilla, amesema kitendo cha kuwapiga faini ni moja ya njia na fundisho sahihi kwa wale wanaoendelea wanaouza na kupandisha bei juu ya Vitakasa Mikono kwa kujipatia faida zaidi na kwenda kinyume na matamko ya Viongozi wa Ngazi za juu.

Amesema kuwa suala la Ugonjwa wa CORONA wafanyabiashara wasiichukulie kuwa ndio njia ya kujipatia vipato badala yake wafuate utaratibu wa bei elekezi ambayo Serikali imeweka kutoka kwa Mamlaka husika ya MSD.

“Tumeanza kuchukua hatua, hii iwe fundisho kwa wale wanaoenda kinyume na Sheria , tayari Viongozi wetu washatoa matamko na maangalizo juu ya kupandisha bei kiholela vifaa vya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA lakini cha kushangaza bado wapo watu ambao sio Wazalendo wanafanya Biashara ya kukomoana katika majanga haya. , leo nimeingia mwenyewe hapa dukani Shiv Pharmaceutical Ltd nikanunua Sanitizer Shilingi 4000 yenye Mills 100 wakati inauzwa Shilingi 2000, haiwezekani wenzetu huko wanakufa kwa ugonjwa huu lakini nyie badala ya kuwasaidia Watanzania wenzenu ndio kwanza mnawakandamiza mnafikiri bei mtakayo weka ni wote wataimudu? Nitoe rai kwa mfanyabiashara yeyote ndani ya Manispaa yangu akienda kinyume na Serikali nitamshughulikia na ikiwezekana kumfutia hata leseni tusicheze mchezo na maisha ya watu Viongozi wanajitahidi kuhamasisha kujikinga nyie mnataka faida mwanzo mwisho tufuate sheria , kanuni na taratibu za Nchi zinavyotaka “ Amesema Sheilla.

Aidha hakuishia hapo, kwani aliendelea na ziara yake ya kukagua vituo vya Mabasi ikiwemo Kituo kikubwa cha mabasi Msamvu pamoja na vituo vidogo vya daladala huku akisisitizia sana kila basi liwe na vitakasa mikono pamoja na maji tiririka na sabuni ili kabla ya mteja au abiria kupanda aanze kunawa na kupuliziwa vitakasa mikono katika kujikinga na Ugonjwa wa CORONA ambapo katika wakati huo pia ameyapiga faini ya Shilingi lakini 100,000/ kwa kila basi ambalo halina vitakasa mikono kwa ajili ya abiria .


“Nimeanza kuridhishwa nafikiri elimu sasa imewafikia lakini bado wapo wengine wanaenda kinyume, hivyo tumechukua hatua za kupiga faini magari ambayo hayana kinga za Ugonjwa huo na kuwaonya vikali kuwapiga faini na kuwapatia elimu zaidi ili abiria wawe salama katika safari zao, niwaombe tena Ugonjwa huu ni hatari sana Wamiliki wa vyombo vya Moto, bodaboda, bajaji , daladala, haisi pamoja na mabasi makubwa hakikisheni vitakasa mikono mnakuwa navyo kabla ya abiria kupanda safisheni magari yenu kwenye siti na sehemu zote abiria wanazoshika mnyunyize dawa na muwanyunyizie mikononi kabla ya abiria kupanda watakao kwenda kinyume tutawashughulikia” Ameongeza Sheilla.

Mbali na kukagua bei za vitakasa mikono na mabasi pia amepata nafasi ya kukagua usafi na mazingira katika Bar ambapo katika ukaguzi huo ameifungia na kuitoza faini Bar moja inayojulikana kwa jina la New Shani Sinema Pub & Restaurant iliyopo Kata ya Boma Mtaa wa Old Dar Street jirani na Kituo cha Daladala Mjini inayomilikiwa na Ndg. Godwin Harrison Mkisi , na kumpa siku 2 kukamilisha usafi wa mifereji inayotiririsha maji machafu.

Naye, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Ikaji Rashid, amesema lengo la ziara hizo za mara kwa mara ni kuona utekelezaji na maagizo kutoka kwa Viongozi wa ngazi za juu kama unafuatwa .

Amesema pamoja na Mkurugenzi kupiga faini lakini wametoa zaidi elimu ya kutosha dhidi ya kujikinga na Ugonjwa wa CORONA na kuwahatadharisha kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wenye tabia ya kukiuka maagizo ya Viongozi kwa makusudi.

“Zoezi linakwenda vizuri asilimia 80 watu wameitika lakini bado wapo watu wachache ambao sio waelewa lakini tulichokifanya ni kuwapiga faini na wale wenye maduka ya Dawa (Pharmacy) tumewachukulia Leseni zao za biashara huku tukiwataka watuonyeshe risiti za mauzo yao za vifaa vya Vitakasa mikono ikiwamo Sanitezer zenyewe, Maski ili tuone nasisi tutoe neon kuliko kila mtu kujiamulia atakavyo , lakini bado tutaendelea kupita duka kwa duka , Mtaa kwa Mtaa kuangalia wale wanaoenda kinyume na maagizo yetu, tunataka Manispaa yetu iwe salama na Ugonjwa huu, niwaombe wafanyabishara hususani wenye maduka ya Dawa kama mtaendelea na tabia hii ya kupandisha bei tutawapiga faini sana na kuwanyang’anya Leseni zenu za biashara” Amesema Dr. Ikaji.

Aidha, amesema ili kuhakikisha zoezi hilo lianfanikiwa kwa asilimia 100 tayari wameshatenga makundi makuu 3 ambapo katika makundi hayo kundi la kwanza lianashughulika na ufuatiliaji wa bei elekezi ya dawa na Vitakasa mikono, na kundi la pili kwa ajili ya kuzunguka katika Nyumba za wageni pamoja na Hoteli zote kubwa kuangalia Vitakasa mikono pamoja na jinsi nguo wanazozitumia katika nyumba hizo zina usalama wa kiasi gani maana lazima zifuliwe kwa uamkini na kundi la mwisho na la tatu linashughulika na kutembelea Mama na Baba lishe kwa ajili ya kutoa elimu zaidi.

 Kwa upande wa Afisa Biashara Manispaa ya Morogoro, Festus Herman, amesema ni marufuku kufanya biashara kinyume na sheria hivyo kila mfanyabisahara afuate taratibu za Leseni yake jinsi inavyomruhusu kufanyabisahara nasio kujipangia bei kiholela

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa