• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO AWATAKA WATUMISHI KUWEKA MALENGO KATIKA UTENDAJI WA KAZI.

Posted on: April 6th, 2020

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka watumishi wa Manispaa ya Morogoro kuweka malengo katika utendaji wa kazi ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi na kuiletea maendeleo Manispaa na Taifa kwa ujumla.


Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa  mafunzo kwa Watumishi  na Watendaji wa Kata kuhusu mfumo wa wazi wa mapitio na tathmini ya Utendaji kazi wa Watumishi wa Umma (OPRAS) yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanaendeshwa kwa njia za majadiliano, maswali na majibu , pamoja na kubadilishana uzoefu .

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo , Lukuba, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha washiriki kujadili umuhimu na namna mfumo wa wazi wa mapitio na tathmini ya Utendaji kazi wa Watumishi wa Umma (OPRAS) unavyofanya kazi , kuwawezesha watumishi ambao ni wasimamizi wa kazi kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kuweka malengo ya utendaji kazi na kuwasimamia watumishi waliopo chini yao katika kuweka malengo ya utendaji kazi , kuwawezesha washiriki kwa vitendo katika kuweka makubaliano ya utendaji kazi , kufanya mapitio ya utendaji kazi ya nusu mwaka na upimaji wa utendaji kazi wa mwaka pamoja na kuongoza majadiliano ya watumishi kuhusu changamoto zao za kiutendaji kazi na mbinu za kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.


Amesema kuwa uanzishwaji wa OPRAS ni hatua muhimu kwa Serikali katika kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma kwa umma.

Aidha, amesema OPRAS ni chombo muhimu cha uwajibikaji kwa kila mtumishi ambacho kinasisitiza umuhimu wa USHIRIKISHWAJI, UMILIKI NA UWAZI ambapo watumishi wanahusisha katika kupanga malengo, utekelezaji, kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa malengo na mchakato wa kufanya mapitio ya utendaji.

Lukuba amesema baada ya mafunzo hayo anatarajia kuwa watumishi wataweza kueleza maana , umuhimu na kanuni za usimamizi wa utendaji kazi (Performance Management ) katika utumishi wa Umma, kuonesha uelewa mpana juu ya mfumo wa wazi wa mapitio na tathmini ya utendaji kazi , uelewa mpana wa kanuni za maadili katika utumishi wa Umma na kuzitekeleza kwa Vitendo katika maeneo yao ya kazi , kubuni njia bora za utoaji wa huduma kwa wananchi na Watumishi wanaowasimamia kwa ufanisi na uadilifu pamoja na kuonesha uelewa na ubunifu katika utunzaji na matumizi ya kumbukumbu kwa ajili ya kufanya maamuzi mbalimbali.



Mbali na usimamizi wa utendaji kazi matokeo ya mfumo huo ni mawasiliano ya mara kwa mara kati ya msimamizi wa kazi na mtumishi, na uelewa wa pamoja wa mahusiano yaliyopo kati ya malengo ya taasisi na yale ya mtumishi binafsi.

“Tumefungua rasmi mafunzo haya kwa watumishi wenu nafikiri kile ambacho kitafundishwa kitawasaidia sana katika utendaji wa kazi , lengo tunataka kuona matokeo chanya , mabadiliko haya ya kutathmini utendaji kazi wa watumishi wa umma yanakwenda sambamba na sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1998 na Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 ambazo zote zinasisitiza uwekaji wa mifumo ya menejimenti ya utendaji bora wa kazi inayojali matokeo ya kazi na kwamba maswala ya ajira, uteuzi na kupandishwa ngazi katika utumishi wa umma yatakuwa kwa ushindani uwazi  unaozingatia sifa, ujuzi na uadilifu wa hali ya juu” Amesema Lukuba.


Mwisho, amesema mategemeo yake ni kwamba mwongozo huo wa OPRAS utatumika kama chombo cha watumishi katika taasisi za umma kujifunza jinsi ya kutumia na kutekeleza OPRAS kwa nia ya kuwa watendaji wanaojali zaidi matokeo bora katika utoaji wa huduma kwa umma.

Kwa upande wa Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro, Waziri Kombo amesema ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa OPRAS unaeleweka kwa pande zote za mwajiri na mwajiriwa, Manispaa ya Morogoro kupitia muongozo wa Serikali imefungua mafunzo haya kuhusu utekelezaji wa OPRAS katika Utumishi wa Umma.

Kombo amesema kuwa, mwongozo huu unatoa tafsiri ya maneno yatumikayo mara kwa mara na unatoa maelezo ya jinsi ya kujaza fomu ya OPRAS na jinsi ya kufanya mapitio na mwisho jinsi ya kutumia matokeo ya mapitio na tathmini ya utendaji kwa mfano utoaji wa zawadi, adhabu na hatua za maendeleo kwa nia ya kuboresha utendaji wa mtumishi.


Katika hatua nyingine, Kombo, amewataka Watendaji wa Kata kupita katika maeneo ya biashara, maduka na vibanda pamoja na maeneo yenye mikusanyiko ya watu ili kuona kama watu wanafuata maelekezo ya wataalamu wa afya katika kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.


Naye Mwalimu wa mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk. Cliford Ringo, amewaomba watumishi kusikiliza kwa uumakini kwa kuwa wao ndio Viongozi wa ngazi za juu hivyo wasipo kuwa na uelewa mkubwa itakuwa vigumu kwenda kuwafundisha wengine huko waendako na kupelekea mfumo huo kuonekana mgumu.



Akitoa mada katika mafunzo hayo, Dk. Ringo, amesema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali katika matumizi ya OPRAS kwa Watumishi wa Umma kitu kinachopunguza ufanisi katika kufikia malengo ya kazi.

Dk. Ringo, amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kutokana na changamoto zilizobainishwa ikiwamo kutokuwepo kwa uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa OPRAS kwa Watumishi wa Umma , kutokuwepo kwa usimamizi thabiti katika kuhakikisha mfumo huo unatekelezwa kama inavyotakiwa pamoja kutokuwepo kwa taratibu madhubuti katika kufanya ufwatiliaji na tathmini.

Mbali na changamoto alizozitaja amesema kuwa changamoto nyingine iliyobainishwa ni suala la ujazaji wa fomu ya OPRAS hususan katika kuweka sahihi wa malengo ya mtumishi unaoshabihiana na upimaji sahihi wa utendaji wa kazi.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa