Mwenge wa Uhuru Umeendelea kukimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro baada ya kupokelewa kutoka Mkoa wa Pwani,ambapo uliweka mawe ya msingi,kufungua miradi,kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo.
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa mnamo tarehe 21/07/2018 ambapo jumla ya miradi 5 yenye thamani ya Bil 6,679,132.00 ilipitiwa na mwenge wa Uhuru.
Katika miradi hiyo 5 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Morogoro wananchi walichangia kiasi cha shilingi 6,258,949,132.00,Halmashauri shilingi 59,450,000.00 na Serikali kuu shilingi 161,179,000,00 ambapo thamani ya miradi yote ni Bil 6,479,578,132.00
Akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Ndg.Charles Kabeho aliwasisitiza wananchi kuwekeza katika Elimu ili kuinua uchumi wa nchi yetu. Aidha, aliwasisitiza wananchi kuhamasika katika shughuli za kiuchumi ili kujiletea maendeleo na kuachana na shughuli zisizokuwa na tija kama kujihusisha na kilimo cha bangi ambayo ni madawa ya kulevya.
Aidha Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 ni "Elimu ni Ufunguo wa maisha Wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu",Kiongozi wa mbio za Mwenge Ndg Kabeho ameendelea kusisitiza wazazi kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kuwapeleka watoto shule .
Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake mkoani Morogoro utakabidhiwa Mkoani Dodoma tarehe 30 Julai, 2018 ili kuendelea na mbio zake mkoani humo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa