• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

POLEPOLE ATAKA ZOEZI LA UHAKIKI WA WAFANYABISHARA SOKO KUU MANISPAA YA MOROGORO KUFANYIKA UPYA

Posted on: January 10th, 2021

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa (Mb), Mhe. Humphrey Polepole, ameuagiza Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kuanza upya zoezi la uhakiki wa Wafanyabiashara waliosajiliwa katika Soko hilo ili kubaini wenye sifa na wasio na sifa.

Kauli hiyo ameitoa Januari 10, 2021 , wakati wa ziara ya kusikiliza na kutatua kero katika Soko hilo mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano katika Manispaa ya Morogoro na mradi wa SGR ambao upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari , Mhe. Polepole, amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kwa kushirikiana na Mstahiki Meya , Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro na Ofisi ya CCM Wilaya kwa kutumia Kamati ya Soko waanze kufanya uhakiki upya wa wafanyabiashara waliosajiliwa katika Soko hilo ili kubaini wale wenye sifa na wasio na sifa.

"Nataka zoezi hili la uhakiki wa kizimba kwa kizimba,fremu mojamoja kwa kila mfanyabiashara ili kuhakikisha kweli ni mtu mmoja na kizimba kimoja au fremu, nafahamu watu waliomba vizimba, na fremu za biashara , na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro alielekeza na kuwakumbusha kwamba ikifika tarehe 5 Januari , 2021, kila mwenye kizimba awe amefika eneo lake, hivyo kwa tarehe aliyotangaza Mkurugenzi na leo ni tarehe 10, sasa tunawatakia kilalakheri wale wenye vizimba ambao hawajafika katika eneo lake. Soko hili ni kubwa sana lakini ni kama ndoo ya maji ina jaa tungetamani kila mtu awe hapa lakini haiwezekani” Amesema Mhe. Polepole.

Mhe. Polepole , ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwamba kwa wale walioshika vizimba viwili uwekwe utaratibu mzuri ili hao waliokosa wapatiwe maeneo ambayo wataweza nao kufanya biashara zao.

Mwisho, amewatahadharisha wale wenye tabia ya kupangisha vizimba kwa mfanyabiashara mwengine kuacha tabia hiyo kabla ya sheria kuchukua hatua kali.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amesema hawatawavumilia wale watakaokutwa wana vizimba zaidi ya viwili kwani licha ya kuwa na kero za msingi na manung’uniko lakini kuna haja ya kuangalia kwa jicho pana changamoto hizo ili pande zote ziweze kuwa kitu kimoja kwa maendeleo ya Manispaa ya Morogoro.

“ Ni kweli kuna changamoto nyingi katika Soko letu, kuna hoja za msingi za wafanyabiashara wa ndani na nje, tumejitahidi kupunguza kero lakini hatukuzimaliza, kama alivyosema mwenezi sasa tunakwenda katika hatua kubwa, hili ni kweli lina changamoto nyingi, lakini tumejitahidi kupunguza kero,lakini nimetengeneza timu kubwa ya kushughulikia kero hizi tunaimani tutazimaliza taratibu taratibu, wiki inayoanza kuanzia tarehe 11 Januari kamati itakuwa hapa kumsikiliza kila mdau lakini nawaomba tuwe wakweli na kuwa waaminifu katika jambo hili ” Amesema DC Msulwa.

DC Msulwa, amesema lazima kazi ifanyike kwakuwa fedha zilizojengea Soko hilo ni za walipa kodi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa