KATIBU Tawala Mkoa wa Morogoro, Dr. Mussa Ali Mussa,amewataka Madiwani kusimamia miradi ya maendeleo katika kata zao ili miradi hiyo kujengwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati.
Kauli hiyo ameitoa Oktoba 27/2022 katika Mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro uliofanyika Ukumbi wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Akizungumza katika Mkutano huo, Dr. Mussa,amesema fedha nyingi zimekuwa zikiletwa na Serikali hivyo Madiwani wanatakiwa kusimamia miradi iliyoko katika maeneo yao ili kuepuka maelekezo mengine watakapochelewesha miradi yanayoweza kusababisha utekelezaji ukawa kwa kiwango cha chini.
’Tushirikiane tuweze kumaliza miradi hii kwa wakati maana ukiwa wa mwisho unaanza kupokea maelekezo mengi sana na kwakuwa timu zote macho yatakuwa kwako unaanza kufanya kwa haraka kwa kulipua kitu ambacho sio sawa’’ Amesema Dr. Mussa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amesema Manispaa imepokea fedha nyingi za ujenzi wa madarasa shilingi Bilioni 1.6 hivyo kama ujenzi huo hautasimamiwa kikamilifu na kuchelewa itakuwa ni kitu kibaya ambacho watakuwa wamemuangusha Rais Samia.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, amewataka wazazi kuchangia chakula kwaajili ya wanafunzi shuleni ili Halmashauri iweze kuwa na maendeleo zaidi kielimu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa