• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

RAS MOROGORO AWATAKA MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO

Posted on: December 14th, 2020

KATIBU Tawala Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalobelo, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo ili kuwezesha Halmashauri kuweza kuongeza uwezo wa kujitegemea kwa mapato ya ndani ya halmashauri.

Kalobelo, ameyasema  hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Madiwani leo Desemba 14,2020 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Stendi ya Mabasi Msamvu.

Amesema kuwa Halmashauri ikiboresha mapato itasaidia kutoa huduma za jamii kwa wananchi ikiwemo afya, elimu, Maji n.k na pia kiwango cha mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake itaongezeka.

Hata hivyo, amewataka Waheshimiwa Madiwani kutenga maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya viwanda vidogo, kati na vikubwa kufanya hivyo kutaongeza Mapato ya halmashauri na Serikali kuu.

Hata hivyo, amesema kuwa ukusanyaji wa mapato ya ndani lazima uendane na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa hiyo ni jukumu la Baraza la Madiwani kusimamia na kuhakikisha kuwa mapato yote yanayokusanywa katika vyanzo vya ndani yanatumika ipasavyo.

“Nitoe rai kwa Manispaa kwamba hakikisheni fedha zinazokusanywa kupitia katika miradi yote zisitumike zikiwa mbichi, bali zinatakiwa kupelekewa benki na kutumika kwa kufuata utaratibu mzuri na ulio sahihi kisheria , “ Amesema Eng. Kalobelo.

Katika hatua nyingine, amewataka Viongozi kuendelea kuhamasisha Wananchi kujiunga na Bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa huku Serikali ikiwa na kazi ya kuhakikisha kwamba Dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa uhakika ili kuendelea kuboresha afya na Ustawi wa Wananchi.

Ufuatiliaji wa mara kwa mara ufanyike ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa na lazima Waheshimiwa Madiwani utaratibu wa kukagua miradi hiyo inayotekelezwa na Halmashauri kupitia kamati zako.

“ Nipongeze Baraza la Madiwani kwa kweli mmefanya vizuri sana katika kipindi cha miaka 5 iliyopita , sasa tunataka uwepo wa Baraza Jipya uwe chachu kubwa ya maendeleo, tutawapima baada ya miaka 5, yapo maendeleo mmeyakuta, tunataka muyaendeleze na kuanzisha mapya, lakini tusisahau wafanyabiashara kuwajengea mazingira mazuri, lazima tuhakikishe kwamba tunajenga kituo cha One Stop Centre kwa ajili ya wafanyabiashara wote” Ameongeza Eng. Kalobelo.

Mwisho, amewataka Madiwani wahakikishe kwamba wanakamilisha Ujenzi wa vyumba 26 vya Ujenzi wa Madarasa mapya na Madawati yake kabla ya mwezi Februari mwakani ili Wanafunzi wapate kukaa na kusoma vizuri.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amewapongeza Manispaa ya Morogoro kwa ufaulu wa Wanafunzi Kidato cha kwanza ambapo kwa Manispaa Jumla ya Wanafunzi 7,577 wamefaulu kujiunga na Kidato cha kwanza.

Amesema kazi iliyopo mbeleni ni kuhakikisha wanatekeleza agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, la kuhakikisha hadi kufikia mwisho wa mwezi wa Februari , mwakani Wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanaanza masomo wakiwa Madarasani  na wakiwa wamekalia Madawati yao.

Msulwa, amesema darasa moja linajumla ya thamani ya Shilingi Milioni 20, hivyo Manispaa itahitaji kutumia Shilingi Milioni 520 kujenga madarasa mapya 26 bila kujumuisha ukamilishaji wa Maboma na samani zake.

“ Ndugu zangu , leo mmekula viapo na mmezindua Baraza jipya , katika agizo hili tuna siku 74, za kujenga Majengo 26 mapya na kumalizia maboma 13 ambapo madarasa hayo yanatakiwa kukamilika na watoto wawe madarasani, hili ni agizo la Serikali ya CCM ambao wote hapa ni Wanachama wake hivyo halina mjadala, niwasihi Waheshimiwa Madiwani, tusianze vibaya kwa kushindwa kutekeleza agizo hili rasmi la Serikali Kuu, kila siku lazima tulifanyie kazi , Mkurugenzi na Madiwani tusikae kimya angalia kama kwenye Kata yako kuna Sekondari, licha ya fedha za Manispaa, lakini tumeandaa utaratibu mzuri wa kukusanya michango kutoka kwa wadau wetu mbalimbali wa maendeleo ili tuhakikishe zoezi hili , peke yetu hatuwezi , ni lazima tushirikiane na Wadau wetu “ Amesema DC Msulwa.

“Nawaomba sana Waheshimiwa Madiwani tumpe ushirikiano Mkurugenzi wa Manispaa yetu, katika kipindi kifupi nilichofanya naye kazi nimegundua kuwa mkishikamana naye kasi yetu ya Maendeleo itaongezeka sana, mimi naamini mkitumia uwezo wake na kujiepusha na migongano isiyo na tija, Morogoro itaingia katika hadhi ya Jiji ikiwa mpya kabisa, Hongereni sana Manispaa, chapeni kazi, “ Ameongeza DC Msulwa.

Kwa upande wa Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro, Ruth John, amewataka madiwani hao kuwa na umoja na mshikamano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowasilishwa kwao kutoka kwa wananchi ili kuweza kuzitatua na kuzijadili kwa pamoja.

Ruth, amewataka madiwani wa kata zote kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta Maendeleo katika kwa kushirikiana vyema na Uongozi wa Manispaa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood, amesema atafanya kazi bila ubaguzi wowote hivyo ameomba madiwani wote kumuunga mkono katika harakati za kuleta Maendeleo Jimbo la Morogoro Mjini.

"Tufanye kazi kwa pamoja, mimi siko upande wa mtu yeyote! Bali nahusiana na watu wote kikubwa ni kuleta Maendeleo ndani ya Halmashauri yetu ya Manispaa ya Morogoro na tuvunje makundi kinachotakiwa ni kwenda kuitekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa vitendo kama tulivyo ahidi kwa Wananchi " Amesema Mhe. Abood.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amehimiza umoja na mshikamano baina ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ili kuweza kuwatumikia vyema wananchi wa Manispaa ya Morogoro.

Mhe. Kihanga, amesema baada ya uchaguzi huo kumalizika viongozi wanajukumu na wajibu wa kuwatumikia wananchi wao bila kuchoka ili kuleta maendeleo yao na hatimaye kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa