• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

RAS MTUNGUJA ATOA WITO KWA WADAU WA LISHE KUONDOKANA NA LISHE DUNI.

Posted on: May 23rd, 2022

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja, amewaasa wadau wa Lishe Mkoa wa Morogoro kuunganisha nguvu zao na kuona njia bora ya kukwamua hali duni ya lishe kwa watoto walio chini ya miaka mitano baada ya takwimu kuonesha kuwa zaidi ya asilimia 43% ya Watoto wa umri huo hapa nchini kuwa na udumavu ukiwemo Mkoa wa Morogoro ambao unazalisha vyakula vya kila aina.

Hayo yamebainishwa Mei 23 Mwaka huu wakati wa Kikao cha ufunguzi wa Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi na makuzi ya awali ya mtoto kupitia Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariam Mtunguja, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Katibu Tawala huyo amesema pamoja na kuwa Mkoa wetu haupo ndani ya orodha ya mikoa kumi yenye idadi kubwa ya watoto waliodumaa inasikitisha kuwa bado Mkoa wa Morogoro unatajwa kuwa na hali ya lishe isiyoridhisha hali ywa kua Mkoa wetu kuwa na bahati ya kuzalisha vyakula vya aina mbalimbali.

“Na inasikitisha zaidi kwamba tunazalisha chakula kwa wingi ikiwemo Mahindi, Mpunga, Matunda na Mbogamboga kila kitu tunacho lakini hali ya udumavu wa watoto wetu ni kubwa” amesema Bi. Mariam Mtunguja.



Aidha, Katibu Tawala huyo wa Mkoa, amebainisha changamoto zinazoweza kukabili maendeleo ya ukuaji wa watoto chini ya umri huo ambapo ili mzazi au mlezi aweze kubaini changamoto hizo, anapaswa kuwa karibu zaidi na mtoto kwa kipindi chote cha hatua za ukuaji wake.

“Asilimia 43% ya watoto wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu na maendeleo ya ukuaji wao, kwa kusababisha na utapiamlo, kukosekana kwa uhakika wa chakula, miundombinu katika familia msongo wa mawazo, uhaba wa rasilimali pamoja na unyanyasaji wa watoto” amesema Bi. Mariam Mtunguja.

Katika hatua nyingine, Katibu Tawala huyo wa Mkoa kupitia hotuba hiyo ameweka wazi kuwa, maendeleo katika ukuaji wa mtoto ni matokeo ya Afua mbalimbali zinazohusisha wadau wa Sekta tofauti ambazo zina wajibika kutoa afua hizo kwa kuzingatia hali halisi ya huduma za malezi jumuishi kwa watoto wadogo kwa kutumia mifumo ya usimamizi na uratibu wa utoaji wa huduma hizo hapa nchini.

Kwa upande wake Bi. Germana Mung’aho ambaye ni Afisa elimu wa Mkoa wa Morogoro amekemea baadhi ya walimu wanaowafanyia ukatili wanafunzi wa madarasa ya awali kwa kuwaadhibu inapotokea wamechelewa kufika shuleni na kutumia vyumba vyenye hali isiyoridhisha katika kuwafundisha, kwani kufanya hivyo kwa watoto hao ni kuchangia kuwadumaza kiakili na kimwili kwa kuwasababishia msongo wa mawazo na ulemavu kwa ujumla.

Akiwakilisha Wakurugenzi watendaji wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema Bwasi amebainisha kuwa kama watendaji watasimamia vema utekelezaji wa Progamu hiyo kwani malezi shirikishi na jumuishi katika makuzi ya watoto ni kitu cha muhimu katika kuwajengea uelewa wa kiakili na kimwili maishani mwao.



Naye, Afisa Programu wa Shirika binafsi la CHILDHOOD DEVELOPMENT ORGANISATION (CDO) ambalo ni watekelezaji wenza wa Programu hiyo Jumuishi Bw. Innocent Rusomyo ameweka wazi kwamba. Katika kutekeleza Programu hiyo wameanzisha na kutekeleza miradi kadhaa ya kuboresha elimu ya awali ya watoto katika kusaidia makuzi na malezi bora ya watoto ikiwemo mradi “MTOTO WETU TUNU YETU” ambao unatekelezwa katika Halmashauri tatu za Mlimba, Mvomero na Ifakara Mji.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa