MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, ameongoza mamia ya wananchi katika kuwakumbuka mashujaa walipoteza maisha yao wakiutetea,Kuupigania na Kulinda Uhuru wa Tanzania.
Maadhimisho hayo yamefanyika Julai 25-2024 katika eneo la mnara wa Mashujaa jirani na Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza katika sherehe hizo za kumbukizi ya Mashujaa, RC Malima, amesema Mashujaa hao walipambana kwa hali na mali kwa ajili ya kuitetea Nchi ya Tanzania wakiwa katika Maeneo Mbalimbali.Walijizatiti na kujitoa kwa uzalendo mkubwa kwa kuweka rehani Maisha yao kwa ajili ya Tanzania.
RC Malima , amesema Mkoa wa Morogoro unaungana na Watanzania wote kuwakumbuka na kuwaombea kheri kutokana na kujali na kudumisha Misingi ya Amani.
Aidha,RC Malima , amesema kuwa misingi mizuri na imara iliyojengwa wasisi wa Taifa letu baba wa Taifa ,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume,imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa Amani na Utulivu,huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote wa ndani au nje na imepelekea wageni,wakimbizi na watalii kuifanya Tanzania kuwa kivutio na kimbilio.
" Tuendelee kuienzi na kuilinda Amani ya Nchi yetu,wapo wanaosema Kuwa Amani ni sawa na Yai mkononi,ukilivunja hautaweza kuliunganisha kamwe,wengine wanasema kuwa Amani haina bei na ikipotea haina soko la kununua.Tuitunze Amani yetu" Amesema RC Malima .
Miongoni mwa shughuli zilizofanyika ni dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa dini pamoja gwaride maalum kwa ajili ya mashujaa.
Katika maadhimisho hayo, Manispaa ya Morogoro iliadhimisha kwa kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kufanya usafi wa Mazingira katika eneo la JUWATA Stendi ya Bajaji Julai 24-2024.
Kila ifikiapo Julai 25 ya kila Mwaka,Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza Maisha yao wakiutetea,Kuupigania na Kulinda Uhuru wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa