• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

RC SHIGELA APONGEZA MANISPAA YA MOROGORO KUPATA HATI SAFI MWAKA FEDHA 2021/2022

Posted on: June 20th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe.Martine Shigela, ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro  kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwa ni Miaka saba mfululizo kutokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Pongezi hizo amezitoa leo Juni 20/2022 katika Mkutano wa Baraza la kupitia taarifa ya utekelezaji wa Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2020/2021 katika Ukumbi wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro

“Hii inaonyesha Baraza la Madiwani, Mkurugenzi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi CCM Pamoja na wataalamu wote wa Manispaa mnafanya kazi kwa kujituma na kufuata vigezo na malengo mliyojiwekea.”Amesema RC Shigela.

RC Shigela, amesema Miradi ya maendeleo ambayo imeanza na kuendelea ikamilike na huduma kwa wananchi ziendelee kutolewa kwa viwango ili wananchi wazidi kuipenda serikali na kuchangia mapato kwa huduma bora wanazozipata.

Aidha, RC Shigela, amesema kipimo cha watumishi ni jinsi ambavyo tunaweza kusimamia utekelezaji wa Miradi yetu ya Maendeleo, hivyo amewaomba watumishi kufanya kazi kwa badii kusimamia miradi ya maendeleo na kuibua vianzia vipya vya mapato.

Hata hivyo, RC Shigela, ameipongeza Serikali kwa hatua ya kuipa Bajeti yote ofisi ya CAG kama walivyoomba kwani itaongeza ufanisi kwa ngazi ya Taifa na hata kwa Wilaya kwani wakaguzi wa ndani watakuwa na wigo mpana wa kukagua matumizi ya fedha pamoja na majengo ya serikali.

Mwisho, RC Shigela, ameiagiza Manispaa ya Morogoro pamoja Halmashauri zote kutengeneza mazingira ya kutoa elimu ya Uchumi kwa Madiwani ili waweze kuibua vyanzo vipya vya Mapato ,kuviendesha pamoja na kutafuta masoko kutoka sehemu mbalimbali.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwakuwa na hati safi inayoridhisha kwa takribani miaka saba mfululizo.

Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando kwa kusimamia mapato na kudhibiti upotevu wa mapato.

Lengo la Baraza maalum hilo lilikuwa ni kujadili hoja mbalimbali kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali pamoja na kufanyia kazi mapendekezo yaliopendekezwa na ofisi ya CAG.

Ikumbukwe kuwa, Jukumu la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa fedha za Serikali ni kukagua fedha zote za Serikali Kwa mujibu wa Ibara ya 143 ya katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyorejewa 2005) na kifungu cha 45 na 48(1) cha Sheria ya Fedha za Serikali za mitaa No 9 ya 1982 (kama ilivyorejewa 2000) pamoja na kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Ukaguzi No 11 ya mwaka 2008.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa