• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

RC SHIGELA AWAPA KICHEKO WANAWAKE WA KATA YA KINGOLWIRA

Posted on: June 10th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, ameibua furaha na vicheko kwa wakazi wa Kata ya Kingolwira Manispaa ya Morogoro mara baada ya kuruhusu huduma bure kwa Wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Vifijo hivyo vimetokea Juni 08/2022 wakati wa mkutano wa RC Shigela wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi , mkutano ulifanyika eneo la Uwanja wa Ofisi ya Kata jirani na Mahakama ya Kingolwira.

Akizungumza na Wananchi hao waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo, RC Shigela alisema katika afya ya wakinamama na watoto wa umri chini ya miaka ni tano ni muhimu kwasababu wakinamama ndio walezi wa kila siku na watoto ni taifa la kesho.

“ Katika suala la afya ni vyema tukatilia mkazo sana hususani Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan la kutaka huduma hii itolewe bure hswa kwa Wajawazito na watoto chini ya miaka 5, niwaombe msigeuze vitega uchumi , nendeni mkakae chini muangalie upya namna ya kuliweka hili, tunataka tutekeleza huduma hii kama sera ya afya ya Kitaifa inavyosema, ukidaiwa risiti toa pesa harafu niletee risiti hiyo harafu uone kama huyo mtumishi atabakia katika kazi hiyo” Alisema RC Shigela.

Katika hatua nyengine, RC Shigela , alisema lazima Vituo vya afya na Hospitali wahakikishe wanaweka utaratibu mzuri wa kuwa mapokezi sahihi ya wa mama wajawazito ili waweze kupatiwa huduma bora na zinazostahiki.

”Nilirudie hili na kulisisitiza , wakina mama na watoto chini ya Umri wa miaka tano hawatakiwi kulipa gharama yeyote kama alivyo agiza Rais wetu Samia Suluhu Hassan , hiyo ni kwasababu wakina mama wengi wana maisha ya chini sana na pia wanafanya jukumu kubwa la kuongeza taifa letu, kwa vile fedha zinatengwa katika huduma hii sitosikia tenda wakina mama hawa wakilalamika kutozwa fedha “ Amesisitiza RC Shigela.

Miongoni mwa kero zilizosikilizwa na kupatiwa majibu ni pamoja na Elimu, Maji, Umeme , Ardhi , Afya , Miundombinu ikiwamo barabara, madarasaja na stahiki za watumishi.

Mwisho, RC Shigela, amewaomba wananchi wa Mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano mkubwa katika zoezi linaloendelea la Anwani za Makazi pamoja na kujiandaa kikamilifu katika zoezi la SENSA linalotarajiwa kufanyika Agosti 23/2022.

Huu ni muendelezo wa ziara zake za Kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ambapo kwa Manispaa ya Morogoro alianza ziara Kata ya Mkundi, Kihonda, Kingolwira na Tungi huku akitarajia kuzifikia Kata zote 29 za Manispaa ya Morogoro .

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa