• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

TAWASANET YAIKABIDHI MANISPAA YA MOROGORO VYOO VYA KISASA VYENYE THAMANI YA MILIONI 43 SHULE YA MSINGI MGULU WA NDEGE.

Posted on: July 17th, 2024

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya TAWASANET ,imeikabidhi Manispaa ya Morogoro vyoo viwili vya kisasa ikiwemo choo cha wavulana na wasichana shule ya Msingi Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi.

Tukio hilo la makabidhiano ya vyoo limefanyika Julai 17-2024 ambapo katika makabidhiano kilipokelewa na mwakilishi wa Mkurugenzi ambaye ni Mchumi wa Manispaa ya Morogoro , Edward Mwamotela akiongozana na Afisa Elimu Msingi, Gregory Fabian.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi choo hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya TAWASANET , Mhandisi Herbet Kashililah, amesema lengo la TAWASANET ni kuboresha miundombinu ya upatikanaji wa maji safi na salama shuleni ikiwemo pamoja na kuboresha miundombinu ya vyoo ikiwemo ujenzi wa vyoo vya kisasa ambavyo wameendelea kuvijenga katika maeneo mbalimbali nchini.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Edward Mwamotela, amewataka waalimu kwa kushirikiana na wanafunzi kulinda vyoo hivyo vyenye miundombinu ya kisasa ili kiweze kudumu kwa muda mrefu, sambamba na kuzingatia usafi katika matumizi.

Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Gregory Fabian, ameowaomba Wazazi kuwahimiza watoto kwenda shule mara baada ya kupata hedhi kwani mabadiliko hayo yanazuilika wakiwa shuleni kutokana na kuwa na chumba maalum ambacho kitatumika kwa wanafunzi hao wanapoingia kwenye hedhi.

Naye Mratibu wa TAWASANET Taifa,Emmanuel Jackson, amesema vyoo hivyo vimegharimu kiasi cha milioni 43 ambapo miundombinu ya watumiaji wote ikiwemo watu wenye mahitaji maalum imezingatiwa.

Pia, Emmanuel,amesema kwa upande wa vyoo vya wanawake wameweka choo maalum ambacho kitatumika kwa wasichana ambao wameingia hedhi kutokana na mabadiliko ya kimwili.

Aidha, Emmanuel,amesema kuwa tafiti zinaonesha kuwa mtoto wa kike anakosa masomo siku 4 hadi 5 kila mwezi kutokana na ukosefu wa huduma ya vyoo bora na maji salama na safi shuleni ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizosaini mkataba wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo mwaka 2030. Miongoni mwa malengo hayo ni lile lengo namba 4: linalohamasisha kuhusu Elimu Bora, Lengo la 5: linalo hamasisha juu ya Usawa wa Kijinsi na lengo namba 6: kuhusu Maji Safi na Salama.

“Huu ni mwanzo tu bado tuna malengo ya kusaidia na shule nyingine , tunataka vyoo hivi viwe vya mfano hususani upande wa mtoto wa kike, TAWASANET tumeguswa na jitihada hizi, tumeona nasisi tuunge mkono jitihada za Manispaa yetu kwa kuwajengea Choo hiki cha Kisasa ili kuhakikisha mtoto wa kike anawekewa mazingira rafiki anapokuwa shuleni ili aweze kuhudhuria siku za masomo kwa ukamilifu kama ilivyokuwa kwa mtoto wa kiume kwani “Ukimkomboa mtoto wa kike umekomboa Taifa zima” Ameongeza Emmanuel.


                                                                     Vyoo vya kisasa vilivyojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya TAWASANET.

                                                                   Makabidhiano ya taarifa za   ujenzi wa vyoo vilivyojengwa na taasisi ya TAWASANETI.                            


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa