• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

WATENDAJI WA MITAA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA MKATABA WA LISHE.

Posted on: April 20th, 2023

WATENDAJI wa Mitaa Manispaa ya Morogoro wameagizwa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa viashiria vyote vilivyomo katika mkataba wa lishe ili kuleta mabadiliko katika kuboresha hali ya lishe kuanzia ngazi ya kaya hadi jamii nzima pamoja na kuweka utaratibu maalum wa kuadhimisha siku ya lishe kwa kila kata.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Lishe Manispaa ya Morogoro, Jacqueline Mashurano, katika kikao kazi na Maafisa Watendaji wa Mitaa juu ya kukumbushana viashiria vya mkataba wa lishe ngazi ya Mitaa ,katika ukumbi wa Mikutano wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro Aprili 20/2023.

Akizungumza na Watendaji hao wa Mitaa, Mashurano, ameeleza kuwa viashiria vinavyotakiwa kutekelezwa ni pamoja na Watoto kupatiwa chakula mashuleni, wakina mama wajawazito kuhudhuria kliniki ipasavyo na kupatiwa madini joto, Watoto kupatiwa vitamin A, Watoto wenye utapiamlo mkali kupatiwa huduma vituoni na utoaji wa fedha ipasavyo kwa ajili ya afua za lishe.

“Watendaji wote hakikisheni mnasimamia vigezo vya upimaji na vipaumbele vya viashiria vya lishe, na muhakikishe kuwa mnapata taarifa za hali ya lishe kwa Watoto chini ya miaka mitano, kufanya ufuatiliaji wa Watoto walioacha matibabu ya utapiamlo kwa kushirikiana na watoa huduma za afya ngazi ya jamii.” Amesema Mashurano.

Mashurano, amesema kuwa ataendelea kujipanga Zaidi ili kuhakikisha kata zote ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kila kiashiria kinafika asilimia 95 na sio chini ya hapo pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wazazi watambue umuhimu wa kuchangia chakula cha Watoto mashuleni ili kukuza kiwango chao cha lishe, kuongeza usikivu na kupunguza tatizo la utoro kwa wanafunzi.

Naye Mratibu wa iCHF iliyoboreshwa Manispaa ya Morogoro, Saada Mustapha, amesema yapo maagizo ya iCHF ambayo Watendaji wa Mitaa wanatakiwa kuyafanya katika maeneo yao ya kazi.

Miongoni mwa maagizo hayo ni pamoja na kuhamasisha jamii ili kuweza kujiunga na bima ya afya iliyoboreshwa, kufikia lengo la asilimia 10 ya uandikishaji kwa kila Kata/Mtaa.

Kwa upande wa Mratibu wa mradi wa Lishe Endelevu Mkoa wa Morogoro, Mariam Mwita, amesema suala la lishe ni mtambuka hivyo jamii kwa kushirikiana na wadau mbali mbali pamoja na Serikali kuhakikisha wanajenga Vizazi vyenye watoto wenye afya na lishe bora ili kuepuka udumavu.

Utekelezaji wa mkataba wa lishe uliosainiwa utakuwa wa miaka nane kuanzia tarehe mosi Julai 2022 hadi tarehe 30 Juni 2030 kulingana na malengo na shabaha zilizoainishwa katika mikakati ya kitaifa ya muda mfupi, muda wa kati pamoja na muda mrefu ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala na Sera mbalimbali za nchi.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa