Watoto wapatao 8,082,838 wenye umri chini ya miezi tisa hadi umri wa miaka mitano wanatarajiwa kupata chanjo ya Surua na Rubella na wengine millioni 4,041,934 wenye umri wa mwaka mmoja na nusu watapatiwa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza(Polio)
Hayo yamesemwa Octoba 17 mwaka huu na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya Surua,Rubella na Polio kwa mwaka 2019 iliyofanyika kitaifa mkoani Morogoro.
Aidha,Waziri Ummy Mwalimu amesema ,hivi sasa Serikali kupitia Wizara hiyo inatoa chanjo tisa ikiwa ni kinga dhidi ya magonjwa 13 yakiwemo magonjwa ya kifua kikuu,kupooza,kifaduro,donda koo,pepopunda,homa ya ini,Kichomi,uti wa mgongo,mafua makali,kuhara,surua,Rubela na saratani ya mlango wa kizazi.
"Ni dhahiri kuwa haya ni mafanikio makubwa ikilinganishwa na mwaka 1975 tulipokuwa tukitoa chanjo dhidi ya magonjwa matano tu"amesema Waziri Ummy.
Aidha amesema zoezi la kampeni hiyo litagharimu takribani Tsh.Bilioni 11.9 sawa na dola za kimarekani Milioni 4.59 huku lengo kuu likiwa ni kushiriki katika mkakati wa kimataifa katika kutokomeza ugonjwa wa Surua na Rubela ili kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto hapa nchini.
Waziri Ummy amesema tayari Tanzania imefanikiwa kufikia lengo la Milenia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka vifo 104 kati ya vizazi hai 1000 kwa mwaka 2004/2005 hadi vifo 54 kati ya vizazi hai 1000 mwaka 2013.
Naye mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Ketsela Mengistu amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutokomeza magonjwa yanayozuilikakwa chanjo.
Dkt.Ketsela amewataka watanzania kushiriki kikamilifu katika kampeni hizo ili kusaidia kupunguza vifo vya watoto vinavyotokana na magonjwa hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Loata Ole Sanare amesema ,jumla ya watoto 328,462 wanatarajiwa kupata chanjo ya Surua na Rubela huku watoto 136,764 watapatiwa chanjo ya polio mkoa wa Morogoro.
Amesema kampeni hizo hufanyika kila baada ya miaka mitatu ambapo mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2014 wakati chanjo ya Rubela ilipoanza kutolewa kwa mara kwanza ambapo ilianza kwa watoto chini ya miaka 15.
Kampeni hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tano kuanzia Oktoba 17 hadi Ocktoba 21 itakapohitimishwa.Kauli mbiu ya kampeni ni "Chanjo ni kinga,kwa pamoja tuwa kingine"
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa