Kama ilivyoada ,kushiriki mazoezi ya viungo kila jumamosi ya pili ya mwezi.Leo pia Mhe .Mkuu wa Mkoa Dkt Stephen Kebwe amewaongoza mamia ya watu waliojitokeza kushiriki mazoezi hayo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro akiwemo Katibu tawala wa Mkoa Bwn. Cliford Tandali na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo.
Katika salamu zake Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amemwaagiza Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kusimamia viongozi wa chini yake ili kuhamasisha zaidi wananchi wote kushiriki mazoezi hayo yakianzia kwa watendaji wa vijiji/mitaa. Lengo ni kuimarisha afya za wananchi wote na sio watumishi wa umma tu .
Naye Katibu tawala wa mkoa Bwana Cliford Tandali ameutaka uongozi wa Uwanja wa Jamhuri kuboresha uwanja huo ili kuvutia washiriki wa mazoezi na zaidi kuvuta wateja wanaopenda kufanyia mashindano ya michezo yao katika uwanja huo hususani wale wa mpira wa miguu.
Leo mazoezi hayo yalifuatiwa na bonanza la michezo,kulikuwepo na mechi ya mpira wa miguu ambapo mashabiki wa timu ya Simba walipambana na washabiki wa timu ya Yanga, na mashabiki wa Yanga waliwabamiza mashabiki wa Simba mabao mawili .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa