MKURUGENZI waManispaa ya Morogoro, Emmanuel Mkongo, amewataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto katika misingi iliyo bora na sahihiili kuepukana na mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Mkongo, ametoawito huo Desemba 31-2024 wakati wa kugawa zawadi ya Sikukuu yaChristimas na Mwaka Mpya katika Makao ya kulelea watoto ya Dar Ul MusleemOrphanage na Mgolole akiwasilisha zawadi za Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Mhe. Mussa Kilakala.
Aidha,Mkongo, amesema wazazi na walezi wanajukumu lakuhakikisha wanatoa malezi yaliyo bora kwa watoto ili waweze kutimiza ndotozao.
"Ni jukumu la kila mzazi na kila mlezi kuwa ni sehemu yakuwajibika katika kuhakikisha kwamba watoto wanapata malezi yanayo waelekezakuandaa kesho yao ambayo ni bora zaidi, hawa watoto ambao wanalelewa katikamakao haya asilimia kubwa ni wazazi kutotimiza wajibu wa malezi nawengine kukimbia majukumu yao kama wazazi japo wapo ambao wazazi wao wameshatanguliambele za haki na hakuna anayewajibika kuwalea "Amesema Mkongo.
Kwa upande wa Afisa Ustawi Manispaa ya Morogoro,SidinaMathias,amewataka wazazi na walezi kuwakaribu na watoto wao ili kutambua mienendo yao ambayo inaweza kusababishakufanyiwa vitendo vya ukatili.
"Sote tunatambua kuwa watoto wamekuwawahanga wakubwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Njia pekee ya kuwasaidiawatoto ni kuwa karibu yao na ili waweze kuwaeleza viashiria vya ukatili wakijinsia wanavyokabiliana navyo mapema kabla hali haijawa mbaya. Ukatili wakijinsia kwa watoto unawaathiri kimwili, kihisia na kisaikolojia. Baadhi yawatoto wamepoteza ndoto katika maisha yao kutokana na vitendo hivi” AmesemaSidina.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa