• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

WAZIRI JAFO AIPONGEZA MANISPAA MOROGORO KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: January 21st, 2020

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, kwa utekelezaji na usimamizi bora wa Miradi ya maendeleo hususani ile ya Kimkakati.

Pongezi hizo amezitoa  Januari 21, 2020 wakati wa sherehe ya Uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Mji Mpya iliyopo Kata ya Lukobe.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mhe. Jafo, amesema kuwa katika Mkoa wa Morogoro ni Manispaa ya Morogoro pekee imekuwa ikitekeleza maagizo yake kwa ufanisi wa hali ya juu jambo lililomfanya azidi kuisifia miradi pamoja na Uongozi wa Manispaa ikiwamo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Manispaa.

Amesema hatua iliyofikia shule hiyo hadi inazinduliwa ameridhika nayo kwa asilimia 100 na kuwaomba viongozi waendelee kuchapa kazi na kufuata maelekezo ya Viongozi wao wa juu wanapotoa matamko ya kiutendaji.

Aidha amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt John Magufuli, katika mwaka januari 2016 , imekuwa ikitumia takribani Bilioni 23.86 kila mwezi kwa ajili ya elimu bure ,ambapo mwaka 2019 Septemba Bilioni 968 zilipelekwa Mamlaka za Serikali na Bilioni 203.6 zilitumika kwa ajili ya miundombinu ya Shule.

Amesema pesa zote zinazotekeleza miradi mikubwa hapa nchini zimetokana na nguvu ya Rais katika ukusanyaji wa kodi .

Amesema Serikali awali ilikuwa ikikusanya kodi ya Shilingi Bilioni 800 huku ongezeko hilo likizidi kupaa na kufikia Trioni 1.3 hadi Trioni 1.9 ni zaidi ya ongezeko la kodi la kihistoria lakini pesa zote zimekuwa zikielekezwa katika miradi ya maendeleo.

"Nimeridhika sana na shule hii, nataka ujenzi huu uwe mfano kwa Wakandarasi wengine    kwani wamefanya kazi nzuri na kwa wakati, lakini niwaonye wale wanaokusanya pesa  za Seriklai mtaani wairudishe haraka pesa hizo sio mali zao ni za Serikali, tukiwa na mapato makubwa ndivyo tunavyozidi kutekeleza miradi mikubwa kwa ubora wenye viwango vinavyoendana na thamani ya fedha, nawapongeza sana Manispaa ya Morogoro hamkuniangusha mnafanya vizuri sana katika miradi yenu" Amesema  Mhe.Jafo.

Amesema baada ya uzinduzi wa Shule hiyo, kilichobakia ni Uongozi kupambana na ufaulu wa elimu kwani zaidi ya Wanafunzi  Elfu 83 waliofaulu viwango vya madaraja (i-iii) katika matokeo ya kujiunga na kidato cha tano wanatoka katika Shule za Serikali.

Wakati huo huo amepiga marufuku Walimu wanaofundisha katika Shule za Serikali kuacha tabia za kukatiza vipindi  kwenda kufundisha shule binafsi ambapo wakigundulika watachukuliwa hatua za kisheria.

Pia ametoa agizo kwa Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari, kuhakikisha wanapita kila shule na kuangalia walimu wakuu waliodumu kwa miaka 5 hadi 15 bila mafanikio ya madaraja ya juu ya ufaulu washushwe vyeo na kuwa walimu wa kawaida.

Kuhusu Afya, Waziri Jafo, amesema kwa miaka mitano chini ya Mhe. Rais Dkt John Magufuli , wametengeneza vituo vya afya 352 kutoka vituo 118 huku mwaka huu wa fedha wametenga bajeti ya vituo 52 na kufanya vituo hivyo kuwa 404 nchi nzima.

Pia wametengeneza jumla ya Hospitali  67 za Wilaya na kuongeza 3 ambapo mwaka huu wa fedha  wametenga pesa kwa ajili ya kuongeza Hospitali  27 za Wilaya.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe.Loata Sanare, ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, kwa kuwapatia fedha za ukarabati wa Shule kongwe pamoja na miundombinu  ya ujenzi wa Maboma 24 katika shule 12 za Sekondari Manispaa ya Morogoro .

Miongoni mwa Shule Kongwe zilizopatiwa fedha za ukarabati ni pamoja na shule ya Sekondari Morogoro, Kilakala .

Amesema Shule za Sekondari za Serikali katika Mkoa wa Morogoro zipo 184 na binafsi zipo 63.

Amesema ili kufikia viwango vya ufaulu wamewekeana mikakati na waalimu wote wakuu wa morogoro huku miongoni mwao wakishindwa kufikia makubaliano waliyokubaliana watashushwa madaraja na kuwa walimu wa kawaida.

"Haiwezekani Serikali inatumia mabilioni ya fedha harafu tunapata matokeo mabaya, lazima tukimbizane na kupeana mikakati mizito nahisi maamuzi ya kushushwa madaraja yatapelekea walimu wakuu kujituma na kupata matokeo mazuri, tuwe na uchungu na hizi fedha za wanyonge tusiibie serikali yetu kwakuwa bila kufika malengo ni sawa na kumwibia mwajiri wako fedha"Amesema RC Loata.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Regina Chonjo amesema watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha matokeo ya ufaulu kwa wanafunzi yanakuwa mazuri na Wilaya ya Morogoroinaongoza katika ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ijayo.

Pia amewataka waalimu wakuu wasimamie miundombinu ya shule kwani fedha zinazowekezwa katika miradi ya elimu ni nyingi sana.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, amesema shule zitakazo ongoza kuingia 10 bora katika Manispaa ya Morogoro atatoa zawadi ya Shilingi Milioni 10.

Amemuomba Mhe. Jafo kufikilia miundombinu ya barabara za kata tatu zinazoizunguka Shule ya Sekondari Mji Mpya pamoja na kuweka mazingira ya upatikana ji wa Maji .

Pia Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema licha ya uzinduzi wa shule hiyo lakini bado Manispaa imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwamo mradi wa Soko jipya la Kisasa, Stendi Mpya ya daladala Mafiga na uakarabati wa stendi ya daladala Kaloleni .

Pia amemuomba Mhe. Jafo kulifanyia kazi agizo la Mhe. Rais Dkt. John Magufuli baada ya kutoa tamko la Stendi ya Msamvu kurudishwa Manispaa lakini hadi leo tamko lake halijatekelezwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa